30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

NHC kutumia Sh bilioni sita kukamilisha miradi

Nehemia Msechu
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Msechu

Na Elizabeth Mjatta

SHIRIKA la Nyumba La Taifa (NHC) litatumia zaidi ya Sh bilioni sita katika kukamilisha miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na biashara.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemia Mchechu, katika mkutano wa jukwaa la wawekezaji lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Alisema nyumba hizo za kisasa ambazo zitakuwa na vituo vya biashara, zitajengwa katika Mkoa wa Arusha na Dar es Salaam, ambapo alisema nyumba hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba familia nyingi kwasababu ya kuwa na mahitaji yote muhimu.

“Kama unavyoona mkutano huu umewahusisha na wakuu wa mikoa mbalimbali kwasababu wenyewe ni wadau wetu wakubwa katika masuala ya ardhi, leo tunatambulisha kwao miradi yetu mikubwa mitatu ambayo ni mradi wa Sarafi City na Usa River mkoani Arusha na mradi wa Salama City ulioko Kigamboni,” alisema Mchechu.

Alisema miradi hiyo ya kisasa imejengwa kwa usanifu mkubwa katika kuifanya mikoa hiyo kuwa kivutio katika mipango miji.

“Hii miradi imejengwa nyumba za kisasa na nzuri kwa biashara, tunataka Dar Salaam na miji mingine mikubwa ijengwe kisasa na iwe na nyumba zilizopangika, lakini pia kujenga nyumba hizi pembezoni ya miji tumelenga pia kupunguza foleni za barabarani kwasababu sasa hivi watu wote wa nje ya mji wanakwenda mjini kwa ajili ya shughuli zao za kutafuta kipato,” alisema Mchechu.

Akizungumza katika jukwaa hilo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema hakuna maendeleo yatakayokuja kwa kuwa na miji isiyopangika vizuri.

Alisema ni vigumu kwa mwekezaji kukubali kuwekeza katika miji isiyopangika vizuri kama ilivyo sasa katika maeneo mengi, hususan jiji la Dar es Salaam.

Alisema kwa sasa jiji la Dar es Salaam linakua kwa kasi na kwamba mwaka mmoja ujao litakuwa na watu wasiopungua milioni 8.6.

Aliwataka wawekezaji kuja kuwekeza katika ardhi ya Tanzania na kuwahakikishia kuwa uwekezaji wao utalindwa na sheria za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles