24 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Agizo la JPM lamfanya meneja Tanroads akeshe akijenga daraja

Francis Godwin -Iringa

SIKU chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutoa agizo kwa mameneja wa Tanroads kuwa endapo barabara au daraja likikatika watakuwa hawana kazi, Meneja wa wakala huo Mkoa wa Iringa, Mhandisi Daniel Kindole amelazimika kukesha akijenga daraja la Ruaha Mbuyuni linalounganisha mikoa ya nyanda za juu kusini.

Akizungumza jana baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kilolo, ikiongozwa na Mkuu wa  Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah kutembelea  usalama wa daraja hilo, alisema mvua kubwa zinazoendelea mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya zimeendelea kuhatarisha usalama wa  daraja hilo.

Alisema kuwa kasi ya maji inayofika katika daraja hilo ni kubwa sana, hivyo yeye na timu yake  wameanza ukaguzi na uangalizi wa daraja hilo ambalo ni daraja tegemeo kwa mikoa ya nyanda za  juu kusini na nchi za kusini.

“Mimi na timu yangu tupo hapa kwa zaidi ya siku nne sasa tunafuatilia mwenendo wa maji maana madhara ya daraja hili kama litavunjika ni kubwa  sana, hivyo tumekuwa tukikesha kufanya kazi usiku na mchana ili kulinda usalama wa daraja.

“Tutaendelea kukesha kulinda daraja ili kuepusha madhara makubwa ambayo yangeweza kujitokeza kwa daraja hilo kama litasombwa na maji haya ambayo kimsingi ni mengi yanayoongezeka siku  hadi siku,”alisema mhandisi huyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo, Aloyce Kwezi alisema mvua hizo zinazoendelea  kunyesha zimeathiri miundombinu mingi huku hali ya uchumi katika wilaya hiyo ikiyumba.

Alisema awali katika miezi kama hii huwa wanakusanya mapato ya ndani kupitia usafirishaji wa mazao mbalimbali ambapo kwa siku wilaya  hiyo ilikuwa ikisafirisha malori ya mizigo zaidi ya 40 lakini kwa sasa ni malori yasiyozidi matano tu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah alisema wakati Serikali ikiendelea  kuchukua tahadhari mbalimbali dhidi ya wananchi na miundombinu, ni vizuri wananchi nao wakachukua tahadhari kwa kuepuka kuendelea na shughuli katika maeneo yaliyozungukwa na maji.

Alisema mvua hizo zimeleta madhara makubwa katika Kata ya Ruaha Mbuyuni na maeneo mengine  baaada ya mashamba ya wananchi kusombwa na maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles