24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

AESH ATISHIA KUZICHAPA BUNGENI

Na Fredy Azzah, Dodoma

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hillary (CCM), Aidha, ameeleza kushangazwa na kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni 15 kati ya Sh bilioni 80 zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na kwamba iwapo serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana mashati bungeni.

Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma leo Ijumaa aprili 6, Aesh amesema fedha hizo zilizotengwa zinatosha kunua mahindi Wilaya ya Sumbawanga pekee.

“Kama mkishindwa kununua haya mahindi msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga mkaja kufungua wakati muda umekwenda na kuweka masharti magumu, nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka tutashikana mashati humu ndani.

“Siyo kazi ya mkulima kuhakikisha nchi haina njaa ni kazi ya Serikali, nashangaa huku mnasema tu tumbaku na pamba, bila mahindi huyo mkulima hawezi kulima hayo mazo yake,” alisema Aesh.

Aeshi pia amezungumzia watumishi wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi akisema mmoja wa Madereva waliofukuzwa kazi alimwendesha mpaka Waziri Mkuu Mstaafu (hakutaja jina la waziri huyo).

“Huyu dereva alikuwa amebakisha miaka mitano tu astaafu, sasa hivi mmemfukuza kazi hana cha kufanya, suala hili mliangalie upya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Serikali haipaswi kulaumiwa kwa kuwafukuza kazi wenye elimu ya darasa la saba. Tunafahamu kuwa, kwa muda mrefu, serikali imekuwa ikiwahimiza watu hawa kujiongezea elimu lakini wakawa wagumu.
    Inakuwaje, kwa mfano, mwalimu wa darasa la saba anaendelea kubaki na darasa hilo muda wote badala ya kujiendeleza? Anapata wapi maarifa na mbinu mpya ya kuwafundisha watoto? Au inakuwaje Mtendaji wa Kata au Kijiji anaendelea kubaki na darasa la saba badala ya kujiendeleza ili kwenda na wakati?
    Japo kuna kauli ya kwamba “ukitaka kumnyima Mtanzania jambo liweke kwenye maandishi”, Wasihurumiwe!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles