23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kerr ataka uvumilivu Simba

kerr kazini simba 34NA MWALI IBRHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amewataka wachezaji wake kuwa wavumilivu kutokana na aina ya mazoezi watakayofanya watakapokuwa kambini visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwaongezea kasi tofauti na ilivyokuwa katika mechi zilizopita.

Ikiwa kambini Simba inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki kujipima nguvu kabla ya kurejea kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa Desemba 12,  mwaka huu katika Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana kocha huyo raia wa Uingereza, alisema anahitaji kuwapa wachezaji wake mazoezi ya nguvu ili kuwaweka fiti zaidi ili waweze kupambana na timu yoyote Ligi Kuu na kupata matokeo mazuri.

Alisema anapenda kuona wachezaji wakiwa na stamina ya kutosha jambo ambalo amekuwa akilisisitiza na kulipa kipaumbele wakati wa mazoezi, kwa kuwa ni lazima kwa kila mmoja kikosini aweze kukabaliana na ushindani uliopo.

“Nataka wachezaji wangu waonyeshe tofauti ligi itakapoendelea tena baada ya kusimama kwa muda, ni lazima wacheze wakiwa na kasi na nguvu ya kutosha bila kuchoka mara kwa mara kama ilivyokuwa katika mechi tulizocheza awali,” alisema.

Akizungumzia viwango vya wachezaji wake tangu walipoanza rasmi mazoezi baada ya kupewa mapumziko ya muda mfupi, Kerr alisema ni vigumu kwa sasa kuelezea uwezo wa mchezaji mmoja mmoja lakini amewataka mashabiki kuvuta subira ili waweze kushuhudia mabadiliko uwanjani.

Mwingereza huyo alisema anaendelea kuwapa programu ya mazoezi wachezaji waliopo kikosini kwa sasa wakati akiwasubiri waliopo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’ iliyofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Ethiopia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles