24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: KUZAA KWA OPERESHENI KUNAOKOA MAISHA

141215_fetalsurgery

WASHINGTON, MAREKANI

WANASAYANSI duniani wamesema kujifungua mtoto kwa njia ya upasuaji kunaimarisha maumbile.

Wanawake wengi wanajifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwa sababu njia ya kizazi kuwa nyembamba.

Watafiti walikadiria kuwa visa ambavyon mtoto anashindwa kupita katika njia ya uzazi vimeongezeka kutoka  30 kwa kila vizazi 1,000 katika miaka ya 1960 hadi visa 36 kwa kila vizazi 1,000 leo hii.

Kabla ya njia hii ya upasuaji kuanza kutumika, wanawake wengi walikuwa wakifariki dunia wakati wa kujifungua.

Lakini pia wanasayansi kutoka Austria walioendesha utafiti huu, walisema vifo vya wanawake wakati wa kujifungua vimepunguzwa kwa sababu ya upasuaji.

Hata hivyo, imegunduliwa kwamba mwanamke aliye na njia nyembamba ya kizazi huenda pia mwanawe wa kike akarithi hali hiyo.

Watafiti walisema visa vya watoto kushindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida vimeongezeka kwa kati ya asilimia 10 na 20.

Utafiti huo umechapishwa na jarida Taasisi ya Taifa ya Sayansi (NAM) ya Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles