27.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA: MSIHIFADHI FEDHA MAJUMBANI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

Na MWANDISHI WETU, MANYARA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa ushauri huo jana wakati akifungua tawi la Benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu, mkoani Arusha akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

“Tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama wao. Hivyo basi, ni vema wakatumia benki mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao kwa ajili ya kutunza fedha zao,” alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia kufunguliwa kwa tawi la benki hiyo wilayani Karatu, Waziri Mkuu alisema unaashiria ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo kwa kuwa benki ni kichocheo cha maendeleo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliushauri uongozi wa benki hiyo kuangalia uwezekano wa kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha wananchi kukopa na kupata faida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo,Wilson Ndesanjo, alisema benki hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mtaji mdogo, jambo linalowasababisha washindwe kufungua matawi katika mikoa mingine.

“Changamoto nyingine ni baadhi ya wateja kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, ambapo hatua za kisheria zikichukuliwa wanakimbilia mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles