25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Nadal hatarini kuikosa Olimpiki

Rafa-NadalRIO DE JANEIRO, BRAZIL

NYOTA wa tenisi nchini Hispania, Rafael Nadal, yuko hatarini kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya muda mrefu.

Bingwa huyo wa medali ya dhahabu mwaka 2008 katika michuano ya wazi ya Ufaransa, alishindwa kushiriki michuano ya Wimbledon kutokana na kuwa majeruhi.

Michuano ya Olimpiki inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho kutwa, hivyo mchezaji huyo ana wasiwasi wa kushiriki michuano hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

“Nina wasiwasi na kushiriki michuano ya Olimpiki kutokana na hali yangu bado kuwa na wakati mgumu, nimekuwa nje ya mashindano kwa miezi miwili sasa na sijafanya mazoezi ya nguvu kwa kipindi hiki chote.

“Kwa sasa nipo nchini Brazil kwa ajili ya michuano hiyo na nitajaribu kufanya mazoezi kwa siku hizi chache nione nitakuwa kwenye hali gani, kama nitakuwa kwenye hali mzuri basi nitashiriki na kama nitakuwa tofauti basi siwezi kushiriki kwa kuwa nitafanya vibaya na kuipotezea matumaini timu yangu,” alisema Nadal.

Bingwa huyo namba tano kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi, alikuwa anatarajiwa kuipeperusha bendera ya taifa la Hispania kwa mara ya kwanza baada ya kukosa katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2012, kutokana na kuwa majeruhi.

Hata hivyo, mchezaji huyo amewataka mashabiki wake na taifa la Hispania kumuombea nyota huyo ili hali yake iweze kuwa katika ubora wake kwa ajili ya kulitetea taifa katika michuano hiyo mikubwa.

“Najua mashabiki wangu wengi wanatamani wanione kwenye michuano hiyo mikubwa, hivyo ni kumuomba Mungu kama nitakuwa katika hali nzuri ili niweze kushiriki kikamilifu.

“Baada ya muda mfupi nitaweka wazi kama nitaweza kushiriki, lakini kwa upande wangu natamani kushiriki kwa ajili ya kuwakilisha taifa,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles