23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mo aanza kumwaga fedha Msimbazi

PIX PG32Na WINFRIDA NGONYANI – DAR ES SALAAM

SIKU chache baada ya Mkutano Mkuu wa Simba kupitisha mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kutoka mfumo wa uanachama hadi ule wa hisa, mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameanza kumwaga fedha Msimbazi.

Mo ambaye ndiye kiini cha mabadiliko hayo ya kimfumo ndani ya Simba kutokana na kuweka wazi uamuzi wake wa kutaka kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo kwa dau la shilingi bilioni 20, jana alikabidhi kiasi cha shilingi milioni 100 kwa uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi ambacho kitasaidia kwenye usajili.

Uamuzi huo wa Mo umekuja siku moja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kumwita mezani kwa majadiliano bilionea huyo kijana, kuangalia jinsi gani ataweza kuisaidia timu katika kipindi hiki cha usajili.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo ofisini kwake jana, Mo alisema yuko tayari kuichangia zaidi endapo uamuzi wa wanachama wa kuendesha klabu kwa mfumo wa hisa utafanywa kwa vitendo.

Nikiwa kama mwanachama nimeona ni vema kuchangia mchakato mzima wa usajili, jambo hili nilikuwa nalifikiria muda mrefu sana,” alisema Mo.

Kwa upande wake, Rais wa Simba ambaye alipokea hundi hiyo, Evans Aveva, alisema fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa usajili wa straika wa kimataifa wa Ivory Coast, Fredrick Blagnon, kutoka klabu ya African Sports ya nchini humo, ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya nchini mwake.

“Tunashukuru kwa kiasi hiki cha fedha ambazo kwa namna moja ama nyingine kitasaidia zoezi letu la usajili, ingawa bado tunahitaji zaidi ya Sh milioni 320, hivyo tunawaomba wadau wengine kujitokeza kutusapoti,” alisema Aveva.

Akizungumzia suala la yeye kudaiwa kukwamisha mabadiliko katika klabu hiyo, Aveva alisema: “Watu wanaposema mimi nakwamisha mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu wananikosea sana, kama mimi ningekuwa sitaki hayo mabadiliko nisingetoa wazo la kuundwa kwa kamati ya watu watano kusimamia mabadiliko.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles