24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Real Madrid yatwaa Kombe la Dunia la klabu

realRABAT, MOROCCO

TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia la klabu, baada ya kuifunga San Lorenzo ya Argentina mabao 2-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Marrakesh, Morocco usiku wa kuamkia jana.

Ubingwa huo umeifanya Real Madrid kuwa na mwaka mzuri kihistoria kwani imechukua taji la nne mwaka huu, likiwemo hilo ambalo imelitwaa kwa mara ya kwanza.

Baadhi ya mataji mengine ambayo Madrid imefanikiwa kutwaa mwaka huu ni yale ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Mfalme (Copa de Rey).
Madrid ilianza kutema cheche zake dakika ya 37 baada ya beki wa timu hiyo, Sergio Ramos, kufunga bao zuri kwa kichwa akimalizia kona iliyochongwa kiustadi na kiungo Toni Kroos, bao ambalo lilisimama hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, walikianza kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 51, lililofungwa na winga, Gareth Bale, bao lililowamaliza kabisa mabingwa hao wa Amerika ya Kusini.

Katika mchezo huo, Ramos, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kutokana na mchango alioutoa kwenye timu yake, licha ya Pepe na Kroos kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Ushindi huo umeendeleza mwendo mzuri wa Real Madrid msimu huu, ambapo kwa sasa imecheza michezo 22 ya mashindano mbalimbali bila kufungwa.

Kocha wa timu hiyo, Muitaliano Carlo Ancelotti, amefurahishwa na ushindi huo na kujivunia kwamba timu yake ni bora duniani kwa sasa.

“Nafurahi kuchukua ubingwa huu, naamini tunamaliza mwaka vizuri kwa kucheza michezo 22 bila kufungwa, lakini bado tutaendelea kujituma ili tuweze kumaliza mwaka vizuri kwa kuwa bado haujaisha. Tunataka msimu wa 2015 uwe wa ushindi kama 2014,” alisema Ancelotti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles