24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

ZUCHU HOME COMING kutikisa Zanzibar Agosti 21

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Msanii wa Bongo Fleva nchini, Zuhura Othuman, maarufu ‘Zuchu’ ameweka wazi kufanya tamasha la ‘Zuchu Home Coming’ Agosti 21, mwaka huu katika uwanja wa Amani Visiwa vya Unguja, Zanzibar atakalowashirikisha wasanii wa visiwa hivyo na wengine kutoka Bara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Zuchu amesema tangu ameachiwa rasmi na lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) amekuwa na shahuku kubwa ya kutaka kufanya tamasha ambalo litaonyesha nia na dhumuni la sanaa anayoifanya.

Zuchu amesema sababu iliyomfanya kwenda kufanya tamasha hilo Zanzibar nikufuatia tamasha lake la kwanza alilolifanya katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam lililofahamika kama ‘I am Zuchu’ kuwa kubwa na lililovutia watu wengi.

“Taswira ya sanaa yangu ilichukuliwa tofauti baada ya mimi kutoka pale Mlimani City kupafomu Shoo kubwa sana, nikasema safari hii sitaenda Mkoa wowote nitarudi nyumbani ili hili jambo likaanzwe nilipotokea.

“Wote tunafahamu kwenye utafutaji unaweza kuishi popote lakini hii hainibagui kwamba mimi ni Mtanzania lakini nimetokea visiwani Zanzibar na nimekulia hapa,” amesema Zuchu.

Mkali huyo wa wimbo Sukari, ametaja sababu za kuita tamasha lake ‘Zuchu Home Coming’ kwamba ameita hivyo kwa kuwa anarudi nyumbani lakini pia anaamini mcheza kwao hutunzwa.

Amesema mwitikio mkubwa wa nyumbani ndiyo utawashtua wengi ambao hawamjui na wanataka kumfahamu.

Zuchu amesema kwenye tamasha hilo atapenda kushiriki na wasanii asilimia kubwa wanaotokea Zanzibar kwa kuwa wana uwezo na haki ya kushiriki katika tamasha hilo.

“Nimeongea nao na wameonyesha ushirikiano mkubwa sana, siku hiyo itapambwa na Ngoma, Benbati, Vidumbaki, Taarabu za zamani na za sasa lakini pia Zenji Fleva ya zamani na sasa.

“Tutakuwa na wasanii wenzangu kutoka bara ambao mnawajua, lengo ni kushirikiana na wenzangu, naamini hakuna cha mmoja kinachofanikiwa kwa ukubwa, cha wengi kinafanikiwa kwa ukubwa,” amesema Zuchu.

Aidha, Zuchu amewashukuru wasanii wenzake wa Zanzibar kwa kumpokea vizuri na ushirikiano waliomuonyesha tangu alipowaomba kushiriki katika tamasha lake Agosti 21, kwenye uwanja wa Amani.

“Tunatangaza rasmi Zuchu Home Coming Shoo na Zantel, narudi nyumbani nina shauku kubwa ya kuwaonyesha tulichojiandaa nacho nitoe shukrani za dhati kwanza kwa Zantel mimi balozi wao wa pasua anga campaign.” amesema Zuchu.

Zuchu

Aidha, msanii huyo ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kumuunga mkono na kuwa naye bega kwa bega kupitia wizara Mama za Mambo ya kale na Utalii, Baraza la Sanaa Zanzibar na Wizara ya Sanaa na Utamaduni Zanzibar.

Ametaja viingilio katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na VIP Sh 30,000 na kwamba ambao watanunua kupitia mtandao wa Zantel itakuwa ni Sh 29,000, daraja la pili Sh 5000 kwa kawaida ukinunua kwa Zantel utaipata kwa Sh4500 na daraja la kawaida Sh 3000 na kwamba tamasha hilo litaanza mchana.

Katika upande mwingine Zuchu amesema tamasha hilo likawe chachu ya maendeleo kwa Zanzibar kitalii, kisanaa, kiukuaji wa biashara, ikainue hamasa kwa wasanii wa Zanzibar.

Pia amesema Julai 24 kutakua na semina kwa wasanii kujifunza mambo mbalimbali ya tasnia jinsi gani wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kuwaingizia kipato, semina itakayotolewa na wataalamu wa masuala ya sanaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles