23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

ZITTO: MAONI YANGU YALILENGA KULINDA HADHI YA BUNGE

 

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) ameieleza Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwa maoni yake mitandaoni yalilenga kulinda hadhi, haki, heshima na madaraka ya bunge.

Zitto ameileza kamati hiyo Alhamisi Septemba 21, mjini Dodoma alikopelekwa alfajiri leo chini ya ulinzi wa polisi kutokana na wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyeaigiza kamati hiyo kumhoji kutokana na kauli yake kuhusu kamati za almasi na tanzanite.

“Tafsiri kuwa maneno yangu kuwa Spika hajafikia viwango vya maspika waliotangulia kabla yake kuwa ni kumdharau si sahihi, maoni yangu hayakulenga kuonyesha dharau, bali yalilenga kutaka Bunge liyalinde yale mambo mazuri yaliyosimikwa na maspika hao wa nyuma katika kuisimamia serikali,” amesema Zitto.

Aidha, Zitto amekiri kuwa maneno aliyoandika mitandaoni ni yake ambayo alitoa kama raia wa Tanzania kwani anaamini kuwa Bunge la 11 limekuwa likifanya kazi kwa kuingiliwa na Serikali huku akitolea mfano kuzuiwa kuonyeshwa kwa bunge moja kwa moja kwa kisingizio cha kupunguza gharama za uendeshaji wa mhimili wa Bunge.

“Kitendo cha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Tanzanite na Almasi kusomwa nje ya Bunge na kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu na Rais bila kuwasilishwa na kujadiliwa Bungeni ili kuwekewa azimio la Bunge. Kitendo hiki kinaifanya Kamati hiyo kuonekana kuwa ya Serikali badala ya Kamati ya Bunge,” amesema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema Kamati imesikiliza maelezo ya Zitto  kuhusiana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

“Kamati imemhoji Zitto amejibu maswali yote aliyotakiwa kuyajibu, Kamati imemaliza kazi yake na kwa mujibu wa utaratibu uliopo ikimaliza kazi inaandaa ripoti na kuipeleka kwa Spika,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles