32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Zitto: Hali ya usalama nchini iko hatarini

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam


Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitaendelea kuwahamasisha Watanzania waendeleze mshikamano wao wa kuwapigania Azory Gwanda, Simon Kanguye na Ben Saanane hadi pale watakapopatikana kama walivyofanya wakati alivyopotea mfanyabiashara Mohammed Dewji aliyetekwa na kuapatikana baada ya siku tisa kwani asingepatikana kama wao wasingepaza sauti.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Oktoba 28, na kiongozi wa chama hicho alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao makuu ya ACT-jijini Dar ambapo amesema mshikamano huo ukiendelea vitendo vya utekaji wa watu vitakomeshwa.

Zitto amesema matukio ya kutekwa watu hao na lile la kupigwa risasi Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu Septemba Saba mwaka jana yanaonesha wazi hali ya usalama wa nchi uko hatarini na hadi sasa hakuna hata taarifa ya uchunguzi wa nani alihusika kufanya tukio hilo.

“Matukio mengi yanatokea yanayohatarisha usalama wa nchi lakini hakuna taarifa za kueleweka zinazotolewa badala yake tunaambiwa ni watu wasiojulikana hawa watu ni akina nani mambo yakiendelea hivi wananchi watakosa imani na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Tunafahamu umuhimu wa vyombo hivi ila kwa haya yanayotokea yanavichafua na kama kuna watu watu wanatumika kuharibu taswira yao basi yanahitajika mageuzi makubwa ili kurudisha imani ya watanzania kwasababu sasa hivi hali ilivo wananchi wana mashaka sana juu ya usalama wao, “ amesema Zitto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles