25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Zaidi ya bilioni 4/- zatolewa na TASAF

RAYMOND MINJA-IRINGA

ZAIDI ya Sh bilioni nne zimetolewa na mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kwa vijiji 95 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Huo ni sehemu ya mpango wa Serikali kutoa nafuu ya maisha kwa kuwainua wananchi wa hali ya chini kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya kaya.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ifyagi, Itulituli na Kitilu vilivyopo wilayani Mufindi wakati wa ziara yake jana ,Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alisema kuwa mwaka 2018 pekee serikali kupitia TASAf imetoa Sh zaidi ya bilioni 1.

Hapi aliwataka viongozi waliopo katika vijiji vilivyopo kwenye mpango huo kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ili fedha zinazotolewa na serikali zilete tija kwa wananchi.

Hapi alisema kuwa Serikali imedhamiria  kuwakwamua wananchi wake katika umasikini kwa kuwapatia ruzuku za miradi mbalimbali ya maendeleo  itakayosaidia kuboresha maisha yao.

“Lengo la mfuko huo ni kuwasaidia wananchi masikini kupitia miradi mbalimbali na ruzuku ili muweze kupata chakula na kusomesha watoto.

“Wale ambao wapo katika mfuko wa TASAF yale manufaa mnayoyapata yawasaidie na ninyi kuwajengea uwezo ili mfikie mahala pa kujitegemea kiuchumi,kama una watoto na unapewa fedha za ruzuku kwa ajili ya kuwasomesha wasomeshe kwa bidii na wafauru ili waweze kukwamua familia zao na kijiji”amesema. 

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mninga, Everin Mbondelo alisema TASAF imebadilisha maisha ya wananchi kwa kiasi kikubwa .

Alisema kupitia fedha za TASAF wananchi wameweza kuboresha makazi yao, kusomesha watoto,kuanzisha shughuli mbalimbali  ambazo zimewasaidia kujiingizia kipato na kujikwamua kiuchumi. 

Naye Diwani wa Kata ya Mninga, Festo Mgina alisema kuwa wametumia jitihada  kubwa kuwaelimisha wakazi wa kata hiyo kutumia vema fedha hizo za maendeleo ya jamii kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

Mgina alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfuko huo wanachi wamebadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kununua mifugo na kubadilisha mazingira ya nyumba zao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles