23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

WENYEVITI WA MITAA WATISHIA KUJIUZULU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WENYEVITI wa Serikali za mitaa nchini wametishia kujiuzulu nyadhifa zao kama Serikali itaendelea na msimamo wake wa kuwanyang’anya mihuri ambayo wamedai kuwa ni vitendea kazi vyao.

Kutokana na hilo, wamemwomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kutoa kauli kuhusu hatua hiyo ya kuwanyang’anya mihuri.

Msimamo huo waliutoa jana katika mkutano wao uliofanyika Dar es Salaam. Pia walitoa saa 24 kwa Katibu Mkuu Tamisemi, Mussa Iyombe, kuwaomba radhi kutokana na barua yake aliyoiandika Novemba 30, mwaka jana.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa wenyeviti hao kutoka Manispaa ya Kinondoni, Juma Uloleulole alisema: “Tunatoa siku saba kwa wakurugenzi wote walioandika barua kwa watendaji wa kata na Jeshi la Polisi kuwataka watupokonye mihuri watuombe radhi.

“Wakikaidi maazimo yetu tutajizulu nchi nzima na uchaguzi uandaliwe upya,” alisema Uloleulole.

Aidha Uloleulole ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kijitonyama kwa tiketi ya Chadema, alisema wanawaomba wenyeviti wa Serikali za mitaa nchini nzima kuunga mkono hoja hiyo kwani kitendo cha kunyang’anywa mihuri ni udhalilishwaji kwao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Madale, Kata ya Wazo, Gratian Mbelwa, alisema mihuri hiyo hawakuvunja ghala la Manispaa ya Kinondoni bali walipewa kama vitendea kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles