24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘WENGI HAWAJUI KUANDIKA WASIFU WAO’

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

VIJANA wengi nchini bado hawawezi kuandika wasifu wao  wanapofikia hatua ya kutafuta ajira na hivyo kujikuta wakiishia kunakili wasifu wa watu wengine, hasa uliowekwa mtandaoni, hatua ambayo imeelezwa kuwa haifai.

Aidha, vijana ambao huhitaji kujiajiri nao hushindwa kutengeneza wazo zuri, kulifanya liwe bora na jinsi gani wanaweza kutumia fursa za kibenki zilizopo kupata mikopo kuendeleza mawazo yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sostenes Kewe, alisema hayo jana, alipozungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa mafunzo ya ujasiriamali na ajira kwa vijana kwa njia ya mtandao uitwao Noa Ubongo.

“Vijana wana ndoto za kupata maendeleo, lakini wengi hujikuta ndoto zao hazitimii kutokana na sababu mbalimbali, kwa mfano wale wanaotaka kutafuta ajira tumegundua hawajui kuandika wasifu wao, matokeo yake wananakili za watu wengine na kukosa kazi.

“Wanaotaka kujiajiri nao hawajui kutengeneza na kuliboresha wazo la biashara, sasa kupitia mpango huu wa Noa Ubongo watapata elimu hii kupitia njia ya mtandao,” alisema.

Kewe alisema utafiti kuhusu Elimu ya Mambo ya Fedha wa mwaka 2014 unaonesha asilimia 58 ya Watanzania hawajibidiishi katika kutafuta taarifa mbalimbali kwa kujisukuma wenyewe.

Alisema utafiti huo unaonesha pia asilimia 68 hawana ule uthubutu wa kutafuta elimu ya mambo ya fedha na hivyo kushindwa kuchangamkia fursa nyingi zilizopo huko.

“Kwa hiyo huu ni wakati mwafaka kwa vijana na Watanzania kwa ujumla kufuatilia vipindi vya Noa Ubongo ili waweze kupata elimu ya kibiashara ambayo itawasaidia kutoka kimaisha,”  alisema.

Naye Nisha Sanghvi wa Khanga Rue Media, alisema wameamua kutumia njia ya mtandao, kwani ni rahisi kuwapata vijana wengi kuwafikishia ujumbe huo walionao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles