27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

WAZEEE CHADEMA WATAKA UWAKILISHI BUNGENI

Na ELIZABETH HOMBO

-DAR ES SALAAM

BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limesema ingawa Rais kapewa nafasi ya katiba kuteua wabunge 10 kuingia ndani ya Bunge,   hakuna hata nafasi moja inayowakilisha wazee.

Limesema ni wakati sasa wa wazee kupatiwa mwakilishi katika Bunge   aweze kuwasilisha matatizo yao kama ilivyo kwa wabunge wanawake na walemavu ambao wana wawakilishi ndani ya mhimili huo.

Vilevile limemwomba Rais John Magufuli kukutana na wazee  kujadiliana na kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Kauli hiyo ilitolewa  Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Roderick Lutembeka alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya wazee duniani.

“Sera ya wazee inataka  wazee wawakilishwe katika ngazi zote za uamuzi lakini   wameshindwa kutumia nafasi hiyo kuteua nafasi ya mwakilishi wa wazee.

“Ila wapo wawakilishi wa vijana, wanawake na walemavu. Hali hii inawafanya wazee washindwe kuwa na mtu wa kuwasemea katika vyombo hivi muhimu vya kufanya uamuzi wa nchi,” alisema Lutembeka.

Alisema wazee wamekuwa hawathaminiwi na kutambulika katika ngazi za uamuzi, afya na ndani ya jamii.

Lutembeka  alisema ni wakati sasa kwa Serikali kupeleka muswada wa sheria ya wazee bungeni   kutekeleza Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003.

Alisema endapo Serikali haitafanya hivyo, wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge watumie kanuni ya Bunge kuwasilisha muswada binafsi kuhusu sheria ya wazee nchini.

Lutembeka alisema: “Tunamshauri Rais Magufuli kukutana na wazee katika kikao cha pamoja ambao hawataogopa kumwambia ukweli ili tuliepushe taifa na madhara makubwa yanayoweza kulipata.

“Wazee ambao tunashauri Rais akutane nao ni wazee kutoka vyama vya siasa, viongozi wastaafu wa dini, wastaafu serikalini na awe tayari kupokea ukosoaji wao na kuufanyia kazi.

“Ukosefu wa dawa, wazee wanapofika katika sehemu mbalimbali za huduma za afya huishia kupewa tu dawa za maumivu kwa kuwa wanatakiwa wahudumiwe bure huambiwa dawa hakuna wakanunue,”alisema.

Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, alisema mchakato huo uliokwama unapaswa kupatiwa ufumbuzi kuleta tija kwa taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

“Umuhimu wa taifa kuwa na Katiba mpya unazidi kuonekana kila siku…Watanzania wanataka Katiba mpya kwa ajili ya kutibu majeraha ya taifa hili,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles