23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili mbaroni kwa kujifanya maofisa wa BoT, kuomba rushwa

Janeth Mushi, Arusha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Arusha, linawashikilia watuhumiwa wawili akiwamo mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Mpya, Seleman Wambura, kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuomba rushwa ya Sh milioni 30.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi, mtuhumiwa mwingine ni Loth Kimaro ambaye pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ya kuomba rushwa ya Sh milioni 30, kujifanya maofisa wa Serikali (BoT) na kushawishi kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kujaribu kutenda kosa.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 28 mwaka huu katika Hoteli ya New Arusha, saa tisa alasiri wakitaka kupokea fedha walizoziomba kwa mtoa taarifa.

“Takukuru ilipokea taarifa kutoka kwa mtoa taarifa akidai amepokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Allen Loiruki, aliyedai amepata namba yake kutoka kwa kijana wake anayefanya kazi katika duka lake la kubadilisha fedha.

“Huyo Allen alidai wao ni sehemu ya kikosi kazi toka BoT kilichopo jijini hapa kwa ajili ya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha na kumshawishi atoe Sh milioni 30 ili amsaidie suala lake lisiendelee na hatua za kisheria pale itakapobainika kuna ukiukwaji wa sheria zinazisimamia biashara ya kubadilisha fedha nchini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles