23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Watendaji wa kata, vijiji watwishwa zigo la madawati

Madawati 5Na Upendo Mosha, Hai

MOFISA watendaji wa kata na vijiji wilayani Hai  wameagizwa kuhakikisha tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari liwe limekwisha  ifikapo Aprili 30 mwaka huu.

Agizo hilo lilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Said Mderu, alipozungumza na maofisa hao  na wakuu wa shule za msingi, sekondari, waratibu elimu kata na wakuu wa idara   wilayani humo   kuwahimizi juu ya uwajibikaji kazini.

Alisema kutokana upungufu mkubwa wa madawati  wilayani humo, watendaji hao wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanalidhbiti tatizo hilo haraka iwezekanavyo.

“Katika shule za sekondari na msingi katika halmashauri yetu tunakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati kutokana na ongezeko la wanafunzi, hivyo nawaagiza mhakikishe ifikapo Aprili 30 mwaka huu tatizo hilo liwe limekwisha,”alisema Mderu.

Alisema katika utekelezaji wa agizo hilo ofisi yake  imenunua mbao  zaidi ya 1,000 za awamu ya kwanza za kutengeneza  madawati 2,000 na kila ofisa mtendaji hana budi kutumia njia mbalimbali kufanikisha azma hiyo.

“Ni vema mkatumia njia mbalimbali ikiwamo  kuwaomba  wahisani wa ndani na nje ya wilaya kusaidia kuondoa tatizo la madawati kwa vile  kwa sasa hii ndiyo changamoto kubwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles