25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania washinda milioni 637 za AGT, Rais Samia awapongeza

Na Mwandishi wetu

Wanasarakasi wawili watanzania ambao ni ndugu, Fadhil Ramadhani na Ibrahim Job, wameshinda kitita cha fedha cha dola za Kimarekani 250,000 sawa na sh 637 milioni baada ya kuibuka washindi wa American Got Talent (AGT) Fantasy League.

Watanzania hao wanaounda kikundi cha sarakasi kinachoitwa The Ramadhani Brothers, waliibuka washindi usiku wa jana Februari 19,2024 kwa kuwashinda wapinzani wao wengine tisa waliofika nao fainali.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram baada ya kutangazwa washindi katika usiku huo, wamesema ni ushindi wa kushangaza kwao na kuwashukuru wote waliowapa sapoti.

Wamesema wanajivunia kutangazwa wabingwa wa dunia wa mashindano, huku wakiwapokeza washindani wenzao ambao wamewafanya wawe bora zaidi.

Katika hatua nyingine Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza washindi hao kutokana na kuitangaza vema Tanzania.

“Pongezi kwa vijana wetu Fadhil na Ibrahim (The Ramadhan Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League, safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine,” amesema Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles