28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wahimizwa kupata elimu pindi benki zinaposhindwa kujiendesha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bima ya Amana imetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye banda lao kupata elimu kuhusu Sekta ya Fedha na utoaji wa amana pindi benki zinaposhidwa kujiendesha.

Akizungumza leo Julai 4, 2023 na jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya biashara ya 47 maarufu Sabasaba, Afisa Mwandamizi wa Bima hiyo, Joyce Shala amesema wanatarajiwa kutoa kiwango kipya cha fidia endapo benki ikishindwa kujiendesha ambapo kiwango hicho kitaanza kutolewa mwaka huu.

Ametoa wito kwa benki ambazo azichukua fidia kujitokeza kuchua amana zao ambazo ni kuanzia Sh milioni 1 hadi 1.5.

“Ikitokea taasisi ya fedha imefungwa kwa benki ambayo inakinga ya amana wateja wao wote watapata kuanzia Sh milioni 1 hadi 7.5 kabla ya kusubiri benki kufilisiwa,” amesema Shala.

Naye, Mhasibu wa Bima hiyo, Beatrice Kallanga amesema kazi yao kuu ni kutathimini na kupokea michango kutoka kwenye benki na taasisi za fedha zinazopokea amana pamoja na kusimamia mfuko ili izidi kukua kwa kuwekeza kwenye zamana za Serikali.

“Tupo hapa kuhamasisha wananchi kuwa na imani na taasisi za kifedha kwani ni sehemu salama kabisa na ikitokea isivyo bahati benki ikishindwa kujiendesha sisi tupo kwa ajili ya kuwalipa amana zao ambazo zilikuwepo kwenye benki pindi benki inafungwa,” amesema Kallanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles