21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

FCC yawataka Watanzania kuwa na uelewa juu ya mikataba ya mikopo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katika kumlinda mlaji Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC) imewataka Watanzania kuwa na uelewa kuhusu mikataba ya mikopo ya benki na kuhakikisha ni sawa kilichoandikwa kwenye mkataba hakiwaathiri wala kuwanufaisha wakopeshaji ndipo asaini kwa hiari na siyo kulazimishwa.

Hayo yamebainishwa Julai 4, mwaka huu na Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio kwenye maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba, ambapo amesema kuwa kushiriki maonyesho hayo kuna maana kubwa kwao.

“Katika kumlinda mlaji, tunaangalia mikataba, wanao kwenda kukopa banki mfano; watu wanaopenda kukopa banki waweze kuingia kwenye mikataba ambayo haiwaathiri na kunufaisha wakopeshaji pekee,” amesema Erio.

Amesema Katika kufanya biashara wanahitaji mitaji na kwenda banki kukopa lakini kuna njia nyingine ambayo ni rahisi na ya haraka zaidi yakuungana na mtu anayeleta mtaji.

Hivyo, wanapitisha mikataba hiyo kuhakikisha kuwa wanaruhusu itumike katika banki hizo.

Erio amesema wanasheria mbili ambazo ni sheria ya ushindani na sheria ya alama za bidhaa nakwamba kazi yao kubwa katika sheria hizo ni kuhakikisha wanafanikisha utendaji wa shughuli za kibiashara na uwekezaji nchini.

Aidha, amesema Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza na kufanya biashara uwepo na wadau kama taasisi inayowezesha biashara.

Ametaja majukumu hayo ni pamoja na kushajilisha na kulinda ushindani wote uliopo, ufanyaji wa biashara katika nchi ambao unaongozwa na misingi ya biashara huria.

“Kwa hiyo tunakuwa na ushindani katika watendaji, sisi kazi yetu ni kuhakikisha washiriki wote katika utendaji wa shughuli za biashara wanafanya bila kuumizana na vurugu ambazo zinawafanya wengine washindwe kufanya shughuli zao.

“Tuna fanya hivyo kwa kuhakikisha shughuli za ushindani hakuna watu wanafanya muungano wa kampuni hatua ambayo wakati mwingine inachochea wengine kushindwa kufanya kazi vizuri.

“Wale ambao tayari wamefanya biashara, FCC ina hakikisha kwamba hawapati vikwazo vyoyote vile vya biashara,” amesema Erio.

Amesema wanawezesha kampuni ambazo zinazotaka kuja kuwekeza nchini kwa misingi ya uzalishaji mkubwa wanaweza kufanya hivyo.

Ameongeza kuwa pamoja na hayo, FCC wana hakikisha bidhaa bandia hazina nafasi nchini kwani wanadhibiti ili zisiingizwe kuuzwa wala zisiingie kwa nia ya kuzalishwa nchini.

“Katika suala la bidhaa bandia tunaongozwa na sheria ya alama za bidhaa kuhakikisha zote zinazoingia nchini na wananchi watumie bidhaa halisi zenye manufaa kwao na zisizoleta athari,” amesema Erio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles