25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Watanzania 52 washinda programu ya wajasiriamali TEF

Abuja, Nigeria

Watanzania 52 wameshinda katika programu ya wajasiriamali Afrika, inayoratibiwa na Taasisi ya Tony Elumelu ya nchini Nigeria.

Kwa ushindi huo, wajasiriamali hao sasa wanakuwa miongoni mwa wajasiriamali 1,000 ambao watanufaika kwa kuwezeshwa zaidi ya Sh milioni 10 ili kuimarisha biashara zao na kuzalisha ajira kwa vijana hususani kwa nchi za Afrika.

Hatua hiyo inatokana na matokeo yaliyotanganzwa mwishoni mwa wiki na Taasisi ya Tony Elumelu (TEF) ambayo ni ya Kiafrika inayoongoza kutoa ushauri na kuwawezesha wajasiriamali kutoka Afrika.

Pamoja na hatua hiyo pia ilitangaza wajasiriamali wa Afrika 3,050 kutoka nchi 54 za Afrika ambao wamejiunga kwenye mzunguko wa tano wa dola za Marekani milioni 100 katika programu ya Ujasiriamali wa TEF.

Matokeo hayo yalitangazwa jijini Abuja baada ya washauri wa maendeleo kuwasilisha mchakato wa uteuzi huo, ambapo kwa mwaka huu zaidi ya watu 216,000 waliwasilisha maombi ikiwa ni ongezeko ya watu 151,000 kutoka mwaka jana.

“Takribani maombi 90,000 yaliwasilishwa na wajasiriamali wanawake ikiwa ni ongezeko la asilimia 45, hii ni ishara ya mkakati wa Taasisi hiyo kufikia usawa wa jinisia.

“Wajasiriamali waliochaguliwa kila moja atapokea Dola za Marekani 5,000 za mitaji ambayo haitarudishwa, upatikanaji wa washauri na wiki 12 ya mafunzo ya biashara yanayohusisha moja kwa moja mahitaji ya wajasiriamali kutoka Afrika.

“Julai 26 – 27, 2019, watakusanyika kwenye Mkutano wa Biashara wa TEF, mkusanyiko mkubwa wa kila mwaka wa wajasiriamali wa Kiafrika na mazingira ya ujasiriamali katika Bara hili la Afrika,” amesema mwasisi wa TEF, Tony Elumelu.

Aidha, katika hotuba yake, Mke wa Rais wa Nigeria, Aisha Buhari, alipongeza jitihada za programu na kuwasisitizia wajasiriamali waliochaguliwa kuchangia maandeleo ya bara la Afrika.

“Nina imani hawa wajasiriamali wa Tony Elumelu watakuwa na msaada mkubwa sio tu Nigeria lakini bara nzima,” amesema.

Akizungumza kuhusu mchakato huo Ofisa Mtendaji Mkuu ajaye Ifeyinwa Ugochukwu, amesema; “Programu ya Ujasiriamali wa Taasisi ya Tony Elumelu, imewawezesha kwa mafanikio wajasiriamali 7,520 katika miaka yake mitano ya kwanza kati ya miaka 10 ya programu.

“Ikitimiza miaka mitano kati ya miaka 10 ya programu, uteuzi wa mwaka huu umehusisha wajasiriamali 2,050 wakisaidiwa na washirika wa Taasisi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles