30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalam Bonde la Wami/Ruvu wawanoa madiwani Tonga na Mzumbe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Timu ya ukaguzi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ikiwa katika ukaguzi wa vyanzo vya maji imeshiriki katika kikao baina ya wananchi na Madiwani wa Kata za Tonga na Mzumbe ambapo mbali na kutoa elimu ya utunzaji maji pia wamepokea malalamiko ambayo wameahidi kuyatafutia ufumbuzi.

Katika ukaguzi wa siku mbili kuanzia Ijumaa Septemba 23, 2022 uliofanyika katika maeneo yanayozunguka Mto Ngerengere unaomwaga maji Mto Ruvu ambao ndiyo tegemeo la chanzo cha maji kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Bodi ya Wami Ruvu kupitia wataalam wake mbalimbali imeahidi kufanyia kazi malalamiko ambayo yametolewa na wananchi ambao wameomba zoezi la usimamishaji matumizi mengine ya maji katika vyanzo lilihitaji kushirikisha ngazi za chini ili wataalam wapewe ushirikiano wa kutosha kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wananchi ambaye hakutaka jina lake kuandikwa ameomba makatazo yote au maelekezo yote juu ya matumizi ya maji yatolewe kwa maandishi na yapelekwe katika Serikali za mitaa ili viongozi watambue na watoe elimu kwa wananchi juu ya utunzaji vyanzo vya maji.

Aidha, wananchi hao waliomba wakulima na wafugaji wote kutambuliwa na kutathimini mazao yaliyo ndani ya hifadhi ya mto ili wapewe fidia na pia wapewe chanzo mbadala cha kunyweshea mifugo kwani wanachangia kupitia ufugaji huchangia miradi ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles