25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

WASTAAFU WALILIA NYONGEZA YA PENSHENI

Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa Ndani wa Serikali, Stanslaus Mpembe
Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa Ndani wa Serikali, Stanslaus Mpembe

Na Editha Karlo – Kigoma

WATUMISHI wastaafu wa Serikali wanaolipwa fedha zao kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, wameitaka Serikali kurekebisha viwango vya malipo ya pensheni wanayolipwa sasa kutokana na kupanda gharama za maisha.

Wakizungumza wakati wa uhakiki wa wastaafu hao, wamesema kiwango wanacholipwa wastaafu waliostaafu utumishi wa umma hakiendani na malipo yanayotolewa kwa waliostaafu hivi karibuni.

Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Shaban Funenge, alisema wastaafu wengi ambao wamestaafu miaka 10 iliyopita, wamekuwa na manung’uniko.

Naye Patrick Maganga, alisema uhakiki huo umekuja wakati mwafaka ambao malalamiko ya wastaafu yamekuwa mengi.

Mwalimu mstaafu, Emilia Maibori alisema mafao ya wastaafu yanapaswa kutolewa kwa wakati mwafaka, badala ya kulalamika kutokana na kucheleweshwa.

Alisema alistaafu kazi mwaka 2005, lakini ameanza kulipwa 2015.

Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa Ndani wa Serikali, Stanslaus Mpembe, alisema zaidi ya mikoa 21 ambayo uhakiki huo umefanyika, mafanikio yamekuwa makubwa.

Alisema licha ya wastaafu wanaojitokeza, pia Serikali imetoa fursa kwa wastaafu ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali kufikiwa na watumishi wanaoendesha uhakiki huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles