23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

WAZIRI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA KIJESHI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi

NA MWANDISHI WETU- Pwani

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya kijeshi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Chuo hicho kitatoa mafunzo maalumu kwa vikundi mbalimbali vya kijeshi ili kuwawezesha kukabilina na ugaidi nchini.

Akizungumza jana, Dk. Mwinyi alisema chuo hicho kinachojengwa eneo la Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa hisani na ufadhili wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China, kitakuwa ishara ya kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

“Uzinduzi wa eneo hili la mradi wa chuo cha kijeshi umekuja kwa muda mwafaka kwani chuo hiki kitatoa mafunzo ya kisasa ya namna ya kukabilina na ugaidi pamoja na wahalifu hapa nchini,” alisema Dk. Mwinyi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawapa uwezo wanajeshi  kupambana na wahalifu na ugaidi kwani vita vya sasa vimebadilika, ni tofauti na zamani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema chuo hicho  kitagharimu dola za Marekani milioni 29 na kitakamilika ndani ya mwaka mmoja.

Alisema chuo hicho kitatoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya kijeshi na kitatoa mbinu mbalimbali za kisasa, namna ya kukabilina na  ugaidi.

Mwamunyange alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa utaratibu wa vikundi mbalimbali ili kufundishwa mbinu mpya za kijeshi kwa kushirikina na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China.

Naye Balozi wa China nchini, Lu Youging, alisema Tanzania na China wamekuwa na ushirikiano mzuri kibiashara na kwenye masuala mbalimbali ya kijamii.

Alisema mradi huo wa chuo unajengwa na Kampuni ya China ya Avic International ambayo inajengwa kwa viwango vya hali ya juu hadi ukamilike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles