23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake watajwa kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, amesema wanawake wamekuwa mabalozi wa kupinga ukatili wa kijinsia na kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kuendeleza kipato chao. Alitoa kauli hiyo leo, Julai 12, wakati akifungua Jukwaa la Wanawake Viongozi katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa.

“Wanawake wanapambana katika uchumi na kushirikiana pamoja ili kuendeleza kizazi kijacho. Pamoja na changamoto zilizopo, leo tuna wanawake marubani, wakandarasi, na wataalamu katika sekta nyingi. Tusikate tamaa,” alisema Mgeni.

Akizungumzia nafasi za uongozi kwa wanawake, alibainisha kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amejitahidi kuhakikisha wanawake wanashiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Ukuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Mahakama, na sekta nyingine.

“Huu ni mfano tosha wa Serikali kutambua mchango wa wanawake katika uongozi na ngazi ya jamii. Siku ya Wanawake Duniani, iliyoanzishwa mwaka 1910 na kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1945, inahamasisha umuhimu wa mwanamke,” aliongeza.

Naibu Spika wa Bunge aliwasifu wanawake kwa jitihada zao katika kujiongezea uchumi na kuzalisha bidhaa zenye soko ndani na nje ya nchi. Pia, alisisitiza umuhimu wa makongamano kama hayo ili kuwapatia elimu nzuri vizazi vijavyo.

Naye, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Latifa Khamisi, alisema kongamano hilo lilikuwa na viongozi mbalimbali na lilijadili mada nyingi ikiwemo sifa za kiongozi mwanamke.

“Wanawake wanapitia changamoto mbalimbali katika uongozi lakini hawatakiwi kukata tamaa. Maonesho ya mwakani yanatarajia kuendelea na kongamano la wanawake kwa lengo la kuwaongezea maarifa katika uongozi wao,” alisema Latifa.

Aliongeza kuwa maonesho hayo yanatarajia kufungwa Julai 13, mwaka huu na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Moro Batiki Group, Dk. Herieth Mkahanga, alisema amejifunza kuwa mwanamke akiwa kiongozi ni lazima ataleta mabadiliko chanya.

“Wanawake wanatakiwa kujiamini na kuondoa mifumo dume ndani ya jamii,” alisisitiza Dk. Mkahanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles