20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

WANAUME WALALAMIKA KUPEKULIWA NA ASKARI WANAWAKE UKUTA MIRERANI

Abraham Gwandu, Arusha.

Utaratibu wa watu kuingia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite ikiwamo askari wa kike wanaolinda ukuta huo kuwakagua wanaume maungoni umelalamikiwa na wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.

Kutokana na hali hiyo, wameiomba serikali kuweka utaratibu mzuri huku wakipendekeza lango kuu la kuingia kuwa wazi kwa saa 24 jambo litakalorahisisha wafanyabiashara, wachimbaji na wafanyakazi wa migodini kutenda kazi zao bila vikwazo.

Wakizungumza na Mtanzania juzi katika eneo la Mirerani wakazi hao waliiomba Wizara ya Madini kujipanga upya na kuweka mfumo mpya utakaowawezesha kuingia ndani ya ukuta huo tofauti na ilivyo sasa.

Mmoja wa wakazi hao ambaye ni mwendesha pikipiki ya kubebea abiria maarufu kama bodaboda katika Mji Mdogo wa Mirerani, Rashid Hamis amedai kupata wakati mgumu wanapotaka kutoka ndani ya ukuta huo, pindi wanapopekuliwa mfukoni tena na askari wanawake.

“Askari wa kike wa eneo hilo wanatupekua mifukoni na kutushika sehemu za siri na kutusababishia mfadhaiko hivyo utaratibu huo ubadilishwe,” amesema.

Akijibu malalamiko hayo, Ofisa Madini Mkazi wa Mirerani, Daudi Ntalima amesema suala la kupekuliwa itabidi liendelee hivyo hadi hapo mfumo wa kamera na vyombo vya kisasa vya upekuzi vitakapowekwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles