22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wanaotetea haki za watoto watakiwa kushirikiana

Na JANETH MUSHI

-ARUSHA

WADAU wanaojihusisha na masuala ya utetezi, ulinzi na malezi ya watoto, wametakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na idara zote zinazoshughulikia watoto ili waweze kuwaokoa na vitendo vya kikatili.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Ofisa Mradi wa Mpango wa kuimarisha familia kutoka Shirika la SOS Children’s Village, Innocent Estomih, wakati akizungumza katika kikao cha pamoja na wadau mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya watoto, kilicholenga kuangalia changamoto zinazowakabili.

Kikao hicho kiliwashirikisha maofisa Ustawi wa Jamii kutoka kata mbalimbali zilizopo Halmashauri ya Arusha, Mkuu wa Wilaya, wanasheria, polisi na wadau wengine.

Alisema kuna changamoto kubwa katika kushughulikia kesi za watoto kutokana na kesi nyingi kukwama polisi, nyingine mahakamani na hata kwa wanasheria.

“Wadau tunaoshughulikia masuala ya watoto, tunapaswa kuungana kwa pamoja ili tujadili namna ya kuwasaidia. 

“Moja ya changamoto ni namna ya kushughulikia kesi za watoto kwenye ushahidi. Kuna wanaokataa kuutoa na kusababisha kesi kukosa nguvu na kuchelewesha haki za watoto,” alisema.

Awali Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata ya Mwandeti, Paulina Masoka, alisema watoto wanahitaji uangalizi mkubwa kwani wengi wanafanyiwa ukatili ila matukio hayo hayaripotiwi.

 “Tunatamani kama kungeanzishwa mahakama maalumu ambayo itakuwa ikishughulikia kesi za watoto ili kuwawezesha wananchi kuripoti kwa wingi matukio hayo kwani wengi wao huogopa kuripoti polisi wakihofia usalama wao, na mahakama hiyo itasaidia haki kupatikana kwa wakati,” alisema.

Kwa upande wake, Wakili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Caroline Shoo, alisema changamoto iliyopo katika kushughulikia kesi za watoto ni kutokuwepo kwa wananchi walio tayari kutoa.

Naye mwakilishi kutoka dawati la jinsia Polisi kutoka kituo cha Ngaramtoni, Lucy Masanga, alisema wamekuwa wakipokea kesi mbalimbali za matukio ya ukatili wa watoto ambapo changamoto kubwa ipo katika kupata ushirikiano wa kutosha, huku mila na desturi zikitajwa kuwa changamoto katika kutatua matatizo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles