29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIKOPO

JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM

WANANCHI wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kupitia mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana (WYDF) ili kujikwamua kiuchumi na kuendana na sera ya Serikali ya kufikia uchumi wa viwanda.

Wito huo ulitolewa juzi na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ilala, Bertha Masagasi, katika semina ya jinsia iliyoandaliwa na mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) kuhusu umuhimu wa mfuko wa WYDF katika uwezeshaji wa wanawake na vijana.

Alisema mfuko huo ambao hutokana na kila halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya uwezeshaji wanawake na vijana ulianzishwa mwaka 1993, lakini kwa Dar es Salaam ulianza kutekelezwa 1998.

“Baada ya harakati mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia, Serikali ya Tanzania ikatoa agizo kwa kila halmashauri kutenga asilimia 5 wa ajili ya wanawake na asilimia 5 nyingine kwa ajili ya vijana, ambapo kwa sasa  inaonesha tumepiga hatua zaidi katika suala la uwezeshaji na tayari kuna mifuko 19 na iliyopo katika Serikali za mitaa.

“Mfuko wa vijana upo chini ya Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na wa wanawake unasimamiwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo, Wazee na Watoto na kundi la mwisho la uwezeshaji wanawake na vijana ambalo lipo chini ya halmashauri, hivyo ni fursa ya vijana walio na umri wa miaka 18 hadi 35 na wanawake wa umri wa miaka 18 hadi 60 kwenda kupata mikopo kwa ajili ya ujasiriamali,” alisema Bertha.

Alisema ili kupata mikopo kituo kinapaswa kuwa na watu 50 sawa na vikundi 10 vya watu watano ambao wana shughuli wanazozifanya, ambapo kima cha chini cha mkopo ni kuanzia Sh 200,000 ambapo cha juu ni Sh milioni 5.

Alisema manispaa hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kuhamasisha wajasiriamali kuwenda kupata mafaunzo SIDO, VETA na UNIDO ili kuongeza ujuzi wao katika shughuli wanazozifanya na hatimaye bidhaa zao ziwe katika viwango vinavyokidhi soko la ushindani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles