24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Bukoba wakerwa na kauli za Lissu kuwatusi viongozi

Na Mwandishi Wetu, Bukoba

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amewatusi marais wastaafu, hayati Benjami Mkapa na mwenzake Jakaya Kikwete kwa kuwaita ni wezi walioshiriki kuiba mali za umma katika utawala wao.

Akizungumza katika Mkutano wa chama hicho uliofanyika Bukoba, mkoani Kagera, Lissu amesema enzi za utawala wao kulifanyika matukio ya wizi na wao wakiwa ni marais wa nchi hii.

Amesema jambo hilo linapaswa kukosolewa bila kujali imani zao na mchango wao katika Taifa letu.

“Tuyazungumze haya majimboni kwetu na tujipange kulinda vya kwetu, kwa sababu mimi nilimsema Rais Mkapa kwa wizi wake na akanikamata na kukaa na kesi miaka sita ingawa Mkapa alikuwa mkatoliki kama mimi lakini yeye alikuwa mwizi japo alitembea na limsalaba lake.

“Sio Mkapa tu, hata huyu naye ni wale wale wezi walioibia nchi yetu na Tegeta Escrow bila kusahau maujambazi mengine aliyofanya katika kipindi cha utawala wake na maujambazi mengine ambapo nilipomsema alinifungulia kesi tatu,” amesema Lissu.

Katika mkutano huo uliofanyika Bukoba, Lissu alitumia muda mwingi kutoa lugha kali dhidi ya viongozi wastaafu akiwamo Hayati Mkapa.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Chadema wameonyesha kuchukizwa na kauli za kiongozi huyo za kuwakashifu viongozi hao.

“Unajua haya mambo mengine nikuwakosea heshima wazee wetu, wamefanya wajibu wao wanapasw kuachwa wapumzike na siyo kuendelea kuna nga majukwaani tena kwa lugha kali namna hii,” amesema Philimoni Kipaka mkazi wa Bukoba.

Upande wake, Restuta John amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kutumia lugha zenye staha wanapokuwa wanataja viongozi wa kitaifa.

“Ni makosa makubwa hasa pale mtu anapomtaja mtu ambaye hawezi hata kuamka kujitetea, hili ni jambo la kuhuzunisha sana, jambo la msingi wanapaswa kufanya siasa za kiungwana kwa kueleza sera zao au kile walicholenga kukisema bila kuumiza viongozi wetu,” amesema Resituta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles