27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 10,000 KUPEWA MIKOPO

Asha Bani


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), imesema wanafunzi 10,196 walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2017/2018, wamechaguliwa kupata mkopo.

Awali bodi hiyo, ilitangaza kuwa wanafunzi 49,282 waliomba mikopo hiyo ili waweze kujiunga na masomo yao ya elimu ya juu.

Taarifa ya HELSB iliyotolewa jana, ilisema wanafunzi hao waliochaguliwa kupata mikopo, ni wa awamu ya kwanza tu.

Ilisema Sh bilioni 34.6 zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196 ambapo, Sh bilioni 108.8 zitatolewa kwa wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza watakaochaguliwa katika awamu zote.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru, ilisema. “Orodha hii ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja.

“Itakumbukwa kuwa moja ya sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji kupata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na Serikali,” ilisema.

Taarifa hiyo ilisema pia kuwa, Sh bilioni 318.6 zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi 3,295 wanaoendelea na masomo wa kuanzia mwaka wa pili na kuendelea.

Alisema tayari Serikali imeshatoa fedha hizo na lengo la bodi ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondoloea wanafunzi usumbufu.

Hivi karibuni, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), ilitangaza awamu ya pili ya udahili wa waombaji wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali kwa maelezo kuwa, waombaji wengi hawajachaguliwa kwa sababu mbali mbali.

Katika taarifa ya TCU walisema kuwa awamu ya pili ya maombi ya vyuo itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye awamu ya kwanza na ya pili.

“Kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba, waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja, wanatakiwa kuamua mara moja kwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika.

“Awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma maombi katika awamu mbili zilizopita), pia waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo kimoja hawatatambuliwa na tume katika udahili wa mwaka 2017/18,” ilisema taarifa hiyo.

TCU iliwataka waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa masuala yote yanayohusiana na udahili badala ya kwenda TCU.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles