25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Wanachama Simba wamtaka Kopunovic

kopunovicNA BARAKA JAMALI, MTWARA

WANACHAMA wa klabu ya Simba Mtwara, wameuomba uongozi wa timu hiyo umrudishe kocha wao wa zamani, Goran Kopunovic, ili kuweza kuirejesha heshima ya timu hiyo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti jana, wanachama hao walisema kuwa uongozi wa timu hiyo umekuwa ukibadili makocha kila mwaka jambo ambalo limewasababishia kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki, pia kumfukuza kocha mzuri Kopunovic.

Wanachama hao walisema suala la kuwafukuza makocha ambao walishaanza kuijenga timu ni jambo la kusikitisha, kwani wanatakiwa makocha wapewe muda na kutolea mfano wa Kopunovic aliyepita kabla ya Dylan Kerr.

Mmoja wa wanachama hao ambaye ni Meneja wa zamani wa Simba, Athman Kambi, amelaani kitendo cha kubadilisha makocha kila mwaka kwani kunapelekea kuharibu mfumo mara kwa mara na wakati mwingine wanamtimua kocha mzuri na kuwaleta ambao hawana uwezo.

“Simba ya sasa hivi ni changa inahitaji kocha ambaye ataijenga timu hiyo hata kipindi cha uongozi wetu tuliijenga timu kwa muda mrefu na kutengeneza mfumo imara ambao uliipatia timu mafanikio ya hali ya juu katika mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu.

“Nafedheheshwa sana na tabia ya kubadili makocha kila wakati, sio kwa Simba tu bali hata kwa timu nyingine  zenye tabia hiyo ila nina amini Simba ni timu changa inahitaji kujengwa kwa muda mrefu na wana Simba tuwe na subira, ila inahitaji kocha mwenye msimamo na kujenga nidhamu ya wachezaji kama Kopunovic,” alisema Kambi.

Naye mwanachama Zubery Mohamed mwenye kadi namba 06067, ambaye pia ni msemaji wa tawi la Mtwara Mjini (Aungurumapo Simba), alisema uongozi wa timu hiyo makao makuu hauna budi kuhakikisha wanamrudisha Kopunovic ili kuweza kujenga heshima ya timu.

“Timu bado inayumbayumba na wachezaji hawachezi kitimu, kuna wachezaji wazuri lakini bado kuna mapungufu ndiyo maana wanachama na wapenzi wa Simba wanamtaka kocha huyo arudishwe kuja kukinoa kikosi hicho.

“Tunajua kabisa kama kocha huyu wa sasa hatufai, tunamhitaji Kopunovic arudishwe ndani ya timu ili aendelee na msimamo wake wa kutopangiwa na mtu katika majukumu yake,” alisema mwanachama huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles