28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Wambura aimwagia sifa Serengeti Boys

 Mchezaji wa timu za watoto wanaolelewa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Mkombo Akim akimiliki mpira.
Mchezaji wa timu za watoto wanaolelewa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Mkombo Akim akimiliki mpira.

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), Michael Wambura, ameipongeza timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kutokana na ushindi mnono wa mabao 6-0 walioupata ugenini dhidi ya Shelisheli.

Serengeti Boys iliyoibamiza Shelisheli mabao 3-0 katika mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, imefanikiwa kutinga raundi ya pili ya michuano hiyo ya kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika kwa Vijana (Afcon 17) kwa jumla ya mabao 9-0.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Bakari Shime, sasa kitavaana na timu ya vijana ya Afrika Kusini ambapo mshindi kati yao atafuzu kucheza fainali za michuano hiyo zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.

Akizungumza na MTANZANIA  jana, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wambura, alisema Serengeti Boys imeliletea sifa kubwa Taifa kutokana na ushindi wa kishindo.

“Ushindi huu haujawahi kutokea kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ambayo imewahi kushiriki mashindano nje ya nchi. Ila wasibweteke kwa matokeo haya kwani wapinzani wao Afrika Kusini ambao watakutana raundi inayofuata ni wazuri kwa kuwa wamewekeza kwenye soka la vijana,” alisema.

Wambura alisema kama kocha Shime ataweka misingi imara kwenye kikosi hicho, kuimarishwa kwa benchi la ufundi Watanzania watarajie  matokeo mazuri kutoka kwa Serengeti Boys.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles