23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu wakuu wahamasishwa kuanzisha klabu za kidigiti shuleni

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, ametoa wito kwa wakuu wa shule za msingi na sekondari kuhamasika kuanzisha klabu za kidijiti ambazo zitazingatia maadili na kubadilisha mwenendo wa vijana nchini.

Akizungumza leo Novemba 2, 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha uwanzishaji na uratibu wa klabu za kidijiti, amesema kuanzishwa kwa kitabu hicho ni muongozo wa vijana kupata fursa ya mapinduzi ya kidijiti.

“Sera ya mwaka 2016 ipo kwenye mchakato wa kubadilishwa ambapo katika hili kimechocheo cha talanta na kuandaa sera ya kampuni changa ambayo itawasaidia kuwa na wadau wakubwa baadaye,”amesema Abdulla.

Amesema kujenga Taifa la kidijitali kupitia klabu hizo zitachangia ufumbuzi na kuwawezesha vijana kuwa wabinifu na wajasiliamali.

Amesema uwanzishaji wa vituo vya ubunifu nchi nzima bila ya kujali elimu waliyonayo kutasaidia kupunguza ukosefu wa ajira na kuziongeza.

“Wakijifunza Tehama wanakuwa bora zàidi na kukuza uchumi na kusaidia mikakati ya kukuza uchumi,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Dk. Jabir Bakari amesema klabu za kidijiti ni majukwaa ya hiari yanayowakutanisha wanafunzi wa rika moja kupata uelewa na kuhamasishana juu ya Tehama uchumi kidijiti na fursa zake.

“Kupitia klabu hizi za kidijiti tunajenga jamii yenye ufahamu wa teknolojia ya kidijiti na iliyo na taarifa na fursa zake “amesema Dk. Bakari

Amesema lengo la uwekezaji kwenye tehama ni kuboresha na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma Kwa wananchi na kuongeza uwezo wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi kidijiti.

“Katika zama hizi ambazo zinajulikana kama zama za mapinduzi ya nne ya viwanda tehama ndiyo nyezo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles