31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Ukonga wahimizwa kupeleka watoto Gisela kwa elimu bora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakazi wa Ukonga, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wametakiwa kupeleka watoto wao shuleni Gisela kwa elimu bora.

Mkuu wa Shule ya Msingi Gisela ambayo ni ya Mchepuo wa Kiingereza, Malimi Kwilasa anasema kuwa shule hiyo imekuwa ikifaulisha kila mwaka kwa wastani mzuri wa daraja A na hivyo kuifanya kuwa moja ya shule bora Wilaya ya Ilala.

Pia shule hiyo ina shule ya awali au chekechea. Anasema matokeo ya mwaka jana darasa la saba shule ilikuwa na watahiniwa 92 kati yao waliofaulu kwa daraja la A ni 85 wakati daraja B ni saba tu.

“Hivyo kwa mantiki hiyo utaona namna shule yetu inayofaulisha, wazazi wawalete watoto wao shuleni hapa,”anasema.

Anasema wakazi wa tarafa ya Ukonga kata ya Kipunguni wana fursa ya kupeleka watoto shuleni hapo ili wapate elimu bora, shule iko Mtaa wa Amani, barabara ya Bombambili.Mwalimu Kwilasa anasema kuwa mazingira ya kufundishia ni bora na shule ina usafiri kwa wanafunzi wa maeneo mbalimbali ya Ukonga na hata nje ya Ukonga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles