24.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wapagazi waanza mwaka kwa kicheko

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Wapagazi wanaofanyakazi ya kubeba mizigo ya wageni katika mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la ‘wagumu’wameuanza mwaka 2024 kwa kicheko ,baada ya misharaha yao kupanda.

Akizugumza mjini Moshimkoani Kilimanjaro Januari 7, 2024 Afisa kutoka Chama cha Wapagazi Tanzania (TPO), Loishiye Mollel amesema mshahara wao umepanda kutoka elfu 20,000 ya awali hadi 25,000.

Amesema kupanda kwa mshahara huo wa wapagazi unatokana na harakati za muda mrefu zilizokuwa zinafanywa na TPO kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo chama cha mawakala wa utalii Tanzania (TATO), Idara ya Kazi pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mwaka 2008 yapata miaka 15, Serikali kupitia Tangazo ya serikali(GN22) ilipandisha mishahara ya wagumu na kufikia dola kumi kwa siku lakini zipo baadhio ya kampuni wakala wa utalii walikuwa wakilipwa chini ya dola kumi kama ilivyopitishwa na Bunge.

Tangu wakati huo wagumu hao wamepitia changamoto nyingi licha ya kufanyakazi ngumu ya kubeba mizigo yenye uzito wa kilo 20 kutoka lango la kupandia hadi juu bila kujarishi nyakati za masika ama kiangazi.

Mawazi kadhaa wenye dhamana na utalii wamepita bila jambo la vijana hawa kupatiwa ufumbuzi na mwaka 2015 mapambano ya kudai nyongeza ya mshahara yalipamba moto kwa usaidizi wa Chama cha Mawakala wa utalii Tanzania(TATO) idara ya kazi, mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Loishiye Lenoy Mollel kutoka Chama cha wapagazi Tanzania(TPO) ndiye aliyetoa tangazo la kupanda kwa mishahara hiyo kuanzia Januari mosi mwaka huu kwa mgumu kulipwa 25,000 kwa siku na malipo haya yatadumu kwa muda wa mwaka mmoja na kuanzia Januari mosi 2025 mishara hiyo itapanda tena hadi kufikia Sh 35,000 kwa siku.

Makubaliano yaliyofikiwa Desemba 29, mwaka jana Mjini Arusha.

“Hii ni habari njema kwa vijana hawa ambao hakika malipo yao hayaendani na kazi ngumu wanayoifanya ndani ya hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro na huu ni mwanzo wa mabadiliko ya michakato mingine ikiwamo suala la mavazi ya kukabiliana na baridi kali ndani ya hifadhi.

Katika kuhakikisha malipo hayo yanafanyika bila longo longo, kila mgumu atalazimika kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi(TIN) itakayomwezesha kufungua akaunti benki na mishahara yao italipwa na wakala kupitia benki.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TATO, Sirili Akko anasema ni jukumu la wagumu kulinda heshima yao kwa kutokukubali kulipwa ujira chini ya viwango vilivyoidhinishwa na kwa kufanya hivyo ni kuwahujumu wenzao pamoja na kuhujumu mapato ya serikali.

Aliongeza kwa suala la ulinzi na usalama kwa mali za watalii pamoja na kuendelea kuuweka katika hali ya usafi mlima Kilimanjaro ili kuendelea kuwavutia wageni.

Wapagazi kwa upande wao wakaiomba TATO kuwadhibiti mawakala utalii wanaoendesha kampuni zao mifukoni ambao wamekuwa chanzo cha kuwapa malipo duni huku baadhi yakidaiwa kununua vocha kwa mawakala wenye leseni ya mlimani (TALA).

“Tuna kesi nyingi sana Idara ya kazi zinazohusu malalamiko ya mawakala wanaowalaghai porters,hatuwezi kuboresha utalii kama tunawalaghai porters,” amesema katibu wa KPA, Salmin Mwita Kerangwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles