23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Waislamu waombwa kutumia mwezi wa Ramadhani kutoa misaada

Na Sheila Katikula,Mwanza

Waumini wa Dini ya Kiislam jijini Mwanza wameombwa kuweka utaratibu wa  kutembelea vituo vya watoto yatima ili waweze  kuwashika mkono kwa kutoa misaada  mbalimbali kwa  mashirika yanayolea watoto hao hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wito huo umetolewa juzi na Sheikh wa Msikiti wa Ibadh uliopo jijini hapa, Nouh Mousa wakati alipotembelea kituo cha Sos Children’s Village Mwanza  kilichopo jijini hapa wilayani Nyamagana kinachotoa malezi na makuzi kwa watoto yatima kutoka  maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Mousa alisema ni vyema wananchi kuweka utaratibu wa  kutoa sadaka kwa watoto hao ambao wamepoteza wazazi wao  ili kuweza kuwapa faraja na kuwapa moyo.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Shabab Daawat Islamiya, Ally Mbarak  alisema lengo la kutembelea  kituo hicho ni kuwatia moyo walezi ambao wanalea watoto hao  ili waweze  kutambua kuwa jamii inawathamini na kuwajali kwa kuona umuhimu wao.

“Tumekuja kuwapa moyo watoto hawa na walezi wao kwani ni jambo jema  kumthamini mtu  mwema ambaye anajali yatima  hata mtume amesema  atakuwa karibu na mja ambaye atakuwa  karibu na  atakaye  msaidia  mtoto yatima.

“Tumetoa sadaka yenye thamani ya sh milion 1  vitume nunua vitu mbalimbali ukiwamo unga wa ngano, mafuta ya kupikia, chumvi, Sabuni, Mchele, sabuni za unga mifuko miwili, maharage, Sukari mifuko miwili tunaamini vitawasaidia kwa kipindi hiki na tunawaomba watu wengine watembelee kotio hiki,” alisema Mbarak.

Naye Afisa wa kituo cha  Child and Youth Development, Masoud Hussein alisema  kituo hicho kina watoto 85 wakiwemo wakike 37 na wakiume 48  na kina watoto wa umri wa miaka miwili hadi 15.

“Sisi tunafanya kazi na Serikali na watoto wao tunawapokea  kutoka kwenye ofisi ya Ustawi wa jamii wanawafatilia kwa kina  wapojilidhisha wanasifa za kuwaleta kwenye kituo chetu wanawaleta na sisi tunawapokea,” alisema Husein.

Kwa upande wake kiongozi wa wanawake wa kituo hicho, Apoche Mwenjesha aliwashrukuru viongozi hao kwa kuona umuhimu wa kuwatembelea watoto hao ambao ni yatima kwani kutoa si utajili bali ni moyo wenye kuamini na kujali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles