29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wafuasi wa Ruto njia panda 2022

NAIROBI, KENYA

AGIZO la Rais Uhuru Kenyatta kuzuia siasa kabla ya mwaka 2022 limewaacha njia panda wanasiasa, ambao wamekuwa wakiandamana na Naibu Rais William Ruto.

Wanasiasa hao, maarufu kama ‘Team Tinga Tinga’ wamekuwa wakiandamana na Dk. Ruto sehemu mbalimbali za hapa kuzindua miradi ya maendeleo, huku wakimfanyia kampeni kama mwaniaji anayefaa zaidi kuchaguliwa na Wakenya kuwa rais.

Hata hivyo, hatua ya Uhuru ya kupiga marufuku wanasiasa hasa wa chama chake cha Jubilee kupiga siasa kipindi hiki, ambayo Dk. Ruto ameiunga mkono kiasi cha kutangaza kujitenga na kundi hilo imewaacha wanasiasa hao katika mshangao.

Hiyo ni kwa kuzingatia kuwa mbali na wengi wao kuapa kufanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba anachaguliwa kuwa rais 2022, baadhi wamekuwa wakijipendekeza kuwa naibu wake.

Kundi hilo linajumuisha Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Kipchumba Murkomen, wabunge Kimani Ichung’wa (Kikuyu), Rigathi Gachagua (Mathira), Ndindi Nyoro (Kiharu), Moses Kuria (Gatundu Kusini), magavana Anne Waiguru (Kirinyaga), Mwangi wa Iria (Murang’a), Francis Kimemia (Nyandarua kwa kutaja wachache.

Kwenye taarifa yake mwishoni mwa wiki, Ruto alikanusha kumpa ruhusa mwanasiasa yeyote kumfanyia kampeni ya urais, akisisitiza kuwa lengo lake ni kumuunga mkono Rais Kenyatta kutimiza Ajenda Nne Kuu za Maendeleo.

“Ninafahamu kuna kundi la watu wanaodai kunifanyia kampeni za urais mwaka 2022. Hata hivyo, hakuna wakati ambapo nishajihusisha wala kumruhusu yeyote kujihusisha katika kampeni hizo kwa niaba yangu.”

“Mimi ni mwanademokrasia anayeamini kuwa kampeni zinafanywa wakati unaofaa pekee,” alisema Ruto, kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, David Mugonyi.

Mbali na hayo, Dkt Ruto aliwaambia wanasiasa hao kuondoa jina lake kwenye shughuli zozote zinazolingana na kampeni za mapema.”

Dk. Ruto pia alionekana kusisitiza hayo Jumamosi alipoandamana na Rais Kenyatta katika Kaunti ya Kajiado, aliposema sasa ataangazia masuala ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles