25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi mwendokasi wasota rumande siku 60

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM



WAFANYAKAZI nane wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka ya Uda-Rapid Transit (UDART), akiwamo kigogo wa Idara wa Fedha wa kampuni hiyo,  wanaendelea kusota mahabusu kwa zaidi ya siku 60 sasa, huku jalada lao likisubiri uamuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Wafanyakazi hao walikamatwa kwa kuhusishwa na mtandao wa kufyatua tiketi feki na kujipatia mamilioni ya fedha huku serikali kupitia Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART ), ikikosa mapato   kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na hali hiyo, inadaiwa   kigogo huyo alikuwa akiongoza timu ya wafanyakazi ambao pia walikuwa wakiuza tiketi za mabasi za wanafunzi za Sh 200 kwa watu wazima huku zile za watu wazima za Sh 650 zikiuzwa mara mbili na hata nyingine zikiwa hazitambuliki kwenye mfumo.

Kukamatwa kwa wafanyakazi hao zaidi ya 30 kulitokana na taarifa zilizoibuliwa na MTANZANIA katika ripoti maalumu Juni mwaka huu.

Ripoti hiyo  ilieleza hujuma mbalimbali  zinazofanywa na wajanja wachache huku serikali ikikosa mapato.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema jalada la kigogo  huyo pamoja na wafanyakazi wenzake saba, bado lipo kwa Mwanashria Mkuu wa Serikali (AG) kwa ajili ya hatua zaidi za sheria.

“Bado tunaendelea kuwashikilia wafanyakazi wa UDART kutokana na tuhuma za uchapishaji wa tiketi feki zinazowakabili.

“Tayari jalada lao lipo mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG)  aweze kuangalia hatua za sheria zitakazochukuliwa na kufikishwa mahakamani,” alisema Mambosasa.

Alisema licha ya jadala hilo kusubiri uamuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikilia wafanyakazi hao kwa hatua zaidi za uchunguzi.

Alisema baada ya kukamilika  uchunguzi na AG kutoa uamuzi wake, wafanyakazi hao watafikishwa mahakamani  waweze kufunguliwa mashitaka kulingana na tuhuma zinazowakabili.

Septemba 24, mwaka huu wafanyakazi zaidi ya 50 UDART, wa vituo vya Kimara na Gerezani   Dar es Salaam, walikamatwa na polisi kwa tuhuma za kutoa tiketi feki kwa abiria wanaoutumia mabasi hayo.

Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa kwa   miezi miwili ilibanika kushuka kwa kasi  mapato ya Kituo cha Kimara kutoka makusanyo ya Sh milioni 20 hadi Sh milioni 25 kwa siku wakati yaliyokuwa yakikisanywa kupitia mfumo wa eletroniki na kufikia hadi Sh milioni 10 kwa siku.

Hatua hiyo iliifanya Serikali kupitia Wakala wa  Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mtandao huo wa wizi huku mmoja wa kigogo wa juu wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART), naye akishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na mtandao huo.

Wafanyakazi hao baada ya kuchujwa  18 walibainika kuhusika moja kwa moja na mtandao huo kwa kilichoelezwa kuendesha vitendo vya uhujumu uchumi katika mradi huo wa serikali.

Inadaiwa wafanyakazi hao kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wengine wanadaiwa kuunda mtandao maalumu wa kufyatua tiketi feki na kujipatia mamilioni ya fedha.

Mradi huo wakati unaanza mwaka 2016, ulikuwa unabeba abiria 75,000 na kwa sasa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 200,000.

Kila safari abiria hutakiwa  kulipa Sh 650 ikijumlishwa  idadi hiyo mapato kwa siku yaliyokuwa yanakusanywa yalikuwa yanafikia Sh milioni 130 ingawa kwa sasa yameshuka.

Katika mtandao huo imebainika mbali ya kufyatua tiketi feki pia wamekuwa wakifanya ujanja kwa kuwauzia watu wazima tiketi za wanafunzi ya Sh 200 badala ya Sh 650 huku kiwango kinachobaki kikingia katika mifuko ya wajanja.

Aprili 24 na Mei 16, mwaka huu makusanyo yalianza kuhujumiwa baada ya UDART kuingilia kati na kutaka kukusanya wao fedha huku wakipinga   tiketi za elektroniki za Kampuni ya Maxcom Afrika Plc.

Hatua hiyo iliifanya UDART kuingilia na kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia tiketi maalumu za mashine ambazozilikuwa zikichanwa na wafanyakazi waliowekwa milango.

Mradi huo ulipoanza, suala la makusanyo lilikuwa chini ya Kampuni ya Maxcom Africa ambao walikuwa wakikusanya kwa mfumo wa elektroniki na udhibiti wa wizi huku UDART wakibaki na uendeshaji mabasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles