23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabishara waanza kununua pamba Simiyu

Derick Milton-Simiyu

Siku mbili baada ya serikali kuwatoa hofu wakulima wa zao la pamba nchini kuwa hadi kufikia Julai 30, 2019 pamba yote iliyoko kwenye maghala itakuwa imenunuliwa, baadhi ya wanunuzi wameanza kununua zao hilo.

Kampuni ya Nsangali iliyoko Wilayani Bariadi, ni moja ya wafanyabishara ambao wameanza zoezi hilo ambapo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Gungu Silanga amesema kampuni yake haitawakopa wakulima pamba yao.

“Tunaishukuru serikali kwa kutusaidia na leo tumeanza kununua pamba, fedha zipo za kutosha tutanunua pamba kwa fedha taslimu na si kuwakopa wakulima, tutanunua kwenye wilaya za Bariadi, Maswa na Itilima mkoa wa Simiyu,” amesema Silanga.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga ameipongeza kampuni hiyo kwa kununua pamba ya wakulima ambayo imejaa kwenye maghala, huku akiitaka kufuata kanuni na sheria za ununuzi wa zao hilo.

Tondoka Jeyeye, ni mmoja wa wakulima katika kijiji cha Sapiwi, aliishukuru serikali kwa kupamba ili kuokoa pamba ya wakulima ambao walikuwa hawajui hatma yao na maisha yao ambayo yanategemea zao hilo kila siku.

Kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa kumekuwa na hali ya kusau sua kwa wafanyabishara kununua zao hilo tangu serikali itangaze msimu mpya wa ununuzi, sababu ikiwa ni kushuka kwa soko la dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles