27.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa Siasa washauri uchaguzi wa Serikali za mitaa kuondolewa TAMISEMI

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini wameshauri uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani usimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na siyo TAMISEMI na uingizwe kwenye sheria ya uchaguzi.

Hayo waliyabainisha leo Septemba 12, jijini Dar es Salaam kwenye siku ya pili ya mkutano Maalumu wa kuthmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi na hali ya siasa nchini uliohushirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Asasi za Kirai, Wanahabari na makundi mengine,

Awai, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Abdul Nondo alisema ili kuwe na uchaguzi huru na haki uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe na TAMISEMI badala yake uingizwe kwenye sheria ya uchaguzi.

“Uchaguzi wa serikali za mitaa uwepo katika sheria ya uchaguzi kuna mswada wa sheria unatarajia kupelekwa bungeni Oktoba na Novemba tunahitaji uchaguzi uwepo kwenye sheria tukifanya hivyo tutakuwa na uchaguzi unaosimamwia na Tume na siyo TAMISEMI,” amesema Nondo.

Amesema msingi wa amani katika demokrasia ni haki, hivyo alishauri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani usisimamiwe na Tamisemi bali Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama ilivyo uchaguzi mkuu.

Naye Mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira alisema amani haitakuwepo kwa sababu kutakuwa na taasisi Maalumu kwa kuwa kuna nchi zina mahakama ya juu, tume huru lakini uchaguzi ukiisha tu amani inatoweka.

Amesema amani ya Tanzania itadumishwa na Watanzania wenyewe kwa kuepuka kauli za kuwagawa wananchi kwa kuwa hakuna demokrasia isiyokuwa na kasoro duniani.

Upande wake Mwenyekiti wa Diaspora, Kelvin Nyamori amesema ili demokrasia itoe haki sawa kwa wagombea wote nyakati za uchaguzi, utaratibu wa kufanya kampeni ubadilishwe kutoka miezi miwili hadi mwaka mmoja ili wagombea wafanye kampeni taratibu na kuwaelimisha wananchi ili wachague viongozi wanaowajua vizuri.

Kiongozi wa Madhebu ya Shia, Sheijhe Hemed Jalala amesema demokrasia nchini hainabudi kuheshimu haki na utu wa Watanzania kwa kutoruhusu mambo yanayokinzana na maadili, mila na desturi za Watanzania.

Mwakikishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Dk. Cammillus Kasala amesema demokrasia ya vyama vingi nchini inatekelezwa kwa shingo upande, hivyo kuna haja ya kurejesha somo la siasa ili wanafunzi wafundishwe misingi ya demokrasia.

Amesema baadhi ya viongozi wa siasa wamejiruhusu kuwa watumwa wa mambo matano ambayo ni mamlaka, faida, sifa, umaarufu na mbwembwe.

Kwa upande wake Askofu Emaus Mwamakula amesema maboresho ya sheria ya Uchaguzi yaende sambamba na maboresho ya baadhi ya vifungu vya Katiba likiwemo Kifungu cha 39(2), 75(5), 74(6) na vinginevyo na pia kianzishwe kifungu kipya cha kuanzisha mahakama ya kuhoji matokeo ya uchaguzi.

Amesema suala la amani na usalama ni nguzo ya msingi na demokrasia ni muhimu kwenye uchaguzi wenye amani.

Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa demokrasia kutahimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi na hali ya siasa nchini unatarajia kufungwa kesho Septemba 13, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles