WABUNIFU wa mavazi chipukizi 25 wanatarajia kuonyesha mavazi yao katika onyesho maalumu la mavazi la ‘Lady in red 2016’ linalotarajia kufanyika Januari 31 katika Ukumbi wa Danken House jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fabak fashions, Asia Idarous, alisema maonyesho hayo kwa mwaka huu yametoa kipaumbele zaidi kwa wabunifu wanaochipukia ili waweze kuonyesha ubunifu wao.
“Mara nyingi katika onyesho kama hili tumekuwa tukiwapa nafasi zaidi wabunifu wakongwe, lakini mwaka huu imekuwa tofauti ambapo wabunifu wengi watakuwa chipukizi huku wakisindikizwa na wabunifu baadhi wakongwe,” alisema.