25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa Habari, Polisi watakiwa kuzingatia misingi ya sheria

Na Malima Lubasha Serengeti

WAANDISHI wa Habari na Askari polisi mkoani Mara, wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Kanuni ili kuepusha migongano baina yao kwa kuwa wote wanategemeana wakati wanatekele za majukumu yao.

Ushauri huo umetolewa na Wakili Daud Mahemba ambaye ni Mwanasheria wakati akichangia hoja kwe nye mdahalo wa Ulinzi na Usalama kati ya Waandishi wa habari klabu ya MRPC  na Askari Polisi mkoani hapa iliyofanyika Musoma.

Wakili Mahemba amesema kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyowekwa kisheri a ikiwamo katiba ya nchi Ibara ya 18 kwa kutumia weledi na taaluma zaidi katika kutekeleza majukumu yao na kutatua changamoto kati yao.

Amesema waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kutafuta habari na kuhabarisha wananchi kwa kuzingatia sheria kinyume chake mwandishi akiandika habari zisizokuwa za kweli zinaweza kuleta migongano kwa wahusika ambapo alisisitiza wasiandike habari inayoleta uchochezi.

Aidha Katibu Tawala Wilaya ya Musoma, Ally Mwendo akizungumza katika mdahalo huo amesema waa ndishi wa habari na Jehi la Polisi wanakutanishwa na majukumu yao,nashauri kwamba kila mmoja atumie weledi hii itasaidia kuboresha mahusiano kwani mna nguvu kubwa sana ya kulinda amani ya nchi na maslahi ya umma.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, James Mnubi ameshauri polisi kutumia weledi Polisizaidi wakati wa kutekeleza wajibu wao hasa wakati wa uchaguzi maana jukumu lao ni kulinda raia na mali zao bila ubaguzi ambapo Mratibu wa Shirika la CWCA Nimrod Swai yeye alisisitiza kila mmoja kuzingatia miiko inayowaongoza pande zote. 

Naye Bishop wa makanisa Daniel Ouma alishauri na kuwataka waandishi kutumia kalamu zao vizuri kwa kuandika habari za maendeleo na kutoa mfano kwake kwamba aliwahi kutishiwa kuwa nitakuandika hali inayoleta hofu kwa wananchi badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na weledi  kupata habari  kutoka kwa jamii  na viongozi.

Awali, SSP Thomas Makene kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salim Morcase kwenye mdahalo huo wa 4 Ulinzi na Usalama kwa Waandishi wa Habari na Polisi mkoani hapa ulioandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) amesema wote wana jukumu la kujenga na kulinda amani ya nchi.

SSP Makene amesema kuwa wakati wa mikusanyiko kama vile mikutano, maandamano, wanapokuwa maeneo hatarishi wakifuatilia habari wawe na vazi la kumtambulisha ili kuwawezeha polisi kuwatambua inapotokea vurugu kama hana utambulisho inakuwa vigumu askari kuwatofautisha na makundi mengine.

“Hivyo, kila upande ukitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maadili sioni kama kuna changamoto yoyote, hivyo kupitia mdahalo huu na vikao vingine vya pamoja itatusaidia kurekebisha changamoto zinazojitokeza wakati wa kutimiza wajibu wetu, tunatakiwa kuboresha mahusiano ili Mara iwe mfano,” amesema.

Makamu Mwenyekiti wa MRPC, Raphael Okelo, amesema kuwa baada ya midahalo ya waandishi wa haba ri na makamanda wa Polisi Tarime Rorya na Mkoa a Mara, hatua ya mwanzo wameunda kamati zinazo husisha pande zote ili kuwawezesha kukutana na kujadili changamoto mbalimbali. 

“Midahalo hii minneni matokeo ya tafiti zilizofanywa na taasisi za kihabari kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari nchini ilibainika kuwa waandishi wanakutana na madhila mengi ikiwemo kupi gwa, kutekwa, kupekuliwa, kupokea vitisho na kuvunjiwa vifaa vya kazi hivyo ili kuweza kufanya kazi vizuri ilibidi kuandaa midahalo na kila upande ukabaini changamoto zake na sasa tunakuja kuweka mambo pamoja nini kifanyike,” amesema Okelo.

Baadhi ya waandishiwa habari wamebainisha kuwa kutapanuliwa wigo na kushirikisha viongozi wa kisiasa na serikali wanaweza kupata suluhisho la migongano baina yao kwa kuwa polisi wamekuwa waki lazimika kutekeleza maagizo yao na kuathiri utaratibu wa wananchi kupata taarifa.                                  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles