27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 7, 2022

Contact us: [email protected]

Vyombo vya habari vinabeba mwelekeo chanya wa taifa-Balozi Boer

Na Faraja Msinde, Mtazania Digital

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe Jakob de Boer ameseam uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu katika kukuza demokrasia ya kweli huku akisisitiza kuwa vyombo vya habari huru ndio msingi wa kuibua mijadala mizito, kutoa muongozo katika utungaji wa sheria na mwelekeo chanya wa taifa.

Warsha ikiendelea.

Balozi Boer ametoa kauli hiyo Alhamisi Oktoba 20, 2022 wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya mabadiliko ya Sheria ya Habari nchini.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), imefanyika katika Hoteli ya Slip Way, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodatus Balile.

Akifungua mkutano huo, Balozi Boer amesema uhuru wa vyombo vya habari ndio moyo wa demokrasia ya nchi yoyote kwa kuwa, hutoa mwanga na mwelekeo wa taifa lolote lile.

“Mamlaka zikijenga tabia ya kusikiliza sauti za watu wote na kuchukua mawazo kwa kiwango kikubwa, itasaidia katika kufanya uamuzi wenye manufaa kwa wananchi na taifa.

‘‘Tunaamini kwamba, uwepo wa tabia ya kusikiliza sauti zote na kusikiliza mawazo ya kila mtu, inawezesha kufanya uamuzi wenye busara kwa manufaa ya taifa sambamba na kuinua maisha ya wananchi wote na taifa kwa ujumla,’’ alisema Balozi Boer.

Awali, akizungumza katika warsha hiyo, Balile alimueleza Balozi Boer juu ya utayari wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta mabadiliko ya sheria ya habari nchini.

Amesema mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari unahusisha taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jamii Forums nakwamba lengo ni kuona tasnia hiyo nyeti nchini ikiheshimika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,670FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles