VYANZO VYA MAJI VYAPUNGUA

0
767

IMG_0633

Na RENATHA KIPAKA – BUKOBA

 MIRADI tisa ya vyanzo vya maji katika wilaya nne za Mkoa wa Kagera, vimepungukiwa maji kwa asilimia kubwa hali inayofanya wananchi wa wilaya hizo kupata maji kwa mgawo na wengine kuyafuata umbali mrefu.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mhandisi wa Mkoa wa Kagera, Vitus Exsavery, alisema vyanzo rasmi na visivyo rasmi vilivyoko katika  vijiji vya wilaya za mkoa huo vimekauka na baadhi vimepungua maji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Alisema upungufu wa upatikanaji maji kwa wananchi hao, unasababisha mgawo baada ya mahitaji ya lita zilizokuwa zikihudumia saa 24 kutokuweza kutoka tena na wilaya ambazo zimepungukiwa maji kabisa ni Biharamulo ambayo ilikuwa na chanzo cha bwawa moja lililokuwa likihudumia wakazi wote limekauka na kubakiwa na tope.

“Mpaka sasa tuliamua kuwagawia maji kwa saa, kwa mfano lita 18,000 zilikuwa zikitoka kwenye chanzo chenye uwezo wa kugawia zaidi ya vijiji vitatu, nyakati hizi maji yanatoka kidogo sana yasiyoweza kuwagawia wote kama ilivyokuwa imezoeleka,” alisema Exsavery.

Alisema Wilaya ya Bukoba ilikuwa ikihudumia vijiji vitatu cha Bonakilovyo, Kitaya, Kabumbilo kutoka kwenye chemichemi kusambaza katika vijiji hivyo imepungua kwa kiwango cha asilimia 80, wananchi hupata maji kwa mgawo.

Alisema katika miradi miwili iliyojengwa kwenye kata ambazo hazipati maji ya Buwasa hutoa maji katika vyanzo vya Kijiji cha Bunkango kilichopo Kata ya Nshabya na Bulibata ambao hutoa maji kwenye chanzo cha Nyamganja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here