22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Vyama vya siasa vifuate sheria-Msajili

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imesema inataka kuviona vyama vinajiendesha kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo ndani ya Ofisi hiy na kwamba kila chama kinatakiwa kifuate taratibu kilizopewa wakati wa usajili.

Akizungumza na Mtanzania Digital Agosti 3, jiji Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Vyama hivyo, Abuu Kimario amesema vyama vya siasa vikijiendesha kwa kufuata taratibu zilizopo hakutakuwa na migogoro ndani ya vyama vyao.

“Vyama vya siasa vifuate taratibu na sheria zilizopo ili kuondoa migogoro ndani na nje ya vyama vyao,”amesema Kimario.

Amesema kazi ya uhakiki siyo kutafuta mchawi ila inataka kujua uhai wa chama na kama kinafuata taratibu zilizopo katika muongozo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Amesema kabla ya kazi ya uhakiki tayari walishatuma madodoso katika vyama vyote vya siasa nchini hivyo maswali wanayowauliza tayari wanayajua.

“Hakuna swali geni tunalowauliza tayari yote yapo katika dodoso tuliowatumia awali,” ameongeza.

Aidha, amesema hivi karibuni ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilionyesha baadhii ya vyama vimepata hati chafu katika mahesabu.

Amesema hati chafu hiyo ilisababishwa na kukosa elimu ya kutunza mahesabu lakini tayari Ofisi ya Msajili ilishatoa elimu baadhii ya vyama na baadhii ya vyama vilikuwa havina namba ya mlipa kodi(TIN) lakini hivi sasa wapo katika utaratibu wa kuipata.

Amesema kazi ya uhakiki hufanyika kila mwaka nchini, lengo ni kuangalia utekelezaji unaofanyika katika vyama hivyo.

“Kazi kubwa ya uhakiki ni kuangalia yale masharti, taratibu na sheria zilizopo zinafuatwa ndani ya vyama hivyo kama vilivyosajiliwa?,” amesema Kimario.

Naye, Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii(CCK), Mchungaji David Mwaijojela ameishukuru ofisi hiyo kuwafanyia uhakiki na kuwaelimisha baadhii ya vitu ambayo walikuwa hawavifahamu ndani ya chama chao.

Mchungaji Mwaijolela amesema wanaiomba Serikali iwapatie ruzuku ili waweze kuendesha chama chao vizuri.

Uhakiki huo ulianza Agosti 2, mwaka huu ambapo tayari imehakiki vyama vya Chadema na CCK.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles