27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Vitambulisho vya JPM vyamtia matatani kigogo wo wa halmashauri

Na Nathaniel Limu-Ikungi 

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, ameagiza Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Paulo Makaka, asimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabali ikiwamo ya upotevu wa vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais Dk John Magufuli.

Makaka anatuhumiwa kupoteza vitambulisho 580 vyenye thamani ya Sh milioni 14 pamoja na upotevu wa kitabu cha leseni chenye namba 801 hadi 900.

Dk. Mwanjelwa alitoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri huyo.

 “Huyu ofisa biashara sio mwaminifu hata kidogo. Naagiza asimamishwe kazi kuanzia leo (10/01/2020) asikanyange ofisini. Mtumishi huyu amechafuka na hasafishiki. 

“Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa) telekelezi majukumu yenu chunguzeni  tuhuma zinazomkabili afisa biashara huyu,” alisema Dk. Mwanjelwa

Aidha aliwataka wakurungezi wa halmashauri nchini, kuchukua hatua stahiki haraka, dhidi ya watumishi ambao wanakwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

“Mkurugenzi au mkuu wa idara asiyekemea uovu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, atakuwa ni sehemu ya uovu husika.

Mkurugenzi au mkuu wa idara, unapashwa uwajue watumishi wako ambao wanafanya mambo kinyume na sheria, kanuni na taratibu. Ukiwatambua washughulikie haraka,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Katika hatua nyingine, aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya nchini, kutenga muda kufanya mikutano ya mara kwa mara kupokea kero zinazowakabili watumishi walio chini yao. Vile vile kupokea ushauri, mapendekezo yatakayotolewa na watumishi hao.

Alisema kuwa mikutano hiyo itasaidia kuimarisha mahusiano mazuri ya karibu, yatakayosababisha kufanya kazi kama timu moja. 

Aliwataka wasiwe miungu-watu, wasikilize changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia majawabu.

Kwa upande wa watumishi wa umma, Dk. Mwanjelwa, amewataka wathamini na kupenda kazi walizopewa. Wachukulie kazi kama fursa, katika ustawi wa maisha yao.

“Niwapongezeni kwa kupata fursa hii ya kuwa watumishi wa umma. Kupitia kazi zenu, mnaaminika mbele ya jamii. Mtumishi wa umma anakopesheka haraka kuliko mtu mwingine. Ninyi ni vioo kwa jamii”,alisema na kuongeza;

 “Lakini baadhi ya watumishi mavazi yao tu yanawaondoa kwenye utumishi wa umma. Watu wanaanza kuulizana hivi huyo ni mtumishi wa umma kweli. Hakikisha unakuwa mtanashati wakati wote na vitendo vyako visiwe vya ajabu ajabu,” alisisitiza.

Wakati huo huo, Dk. Mwanjelwa aliipongeza Halmashauri ya Ikungi kwa kusimamia vema utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles