26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

VIONGOZI 41 SUDAN KUSINI KUSHTAKIWA KWA KUSABABISHA VITA

JUBA, SUDAN KUSINI


TUME ya Umoja wa Mataifa ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini, imesema kuna ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka viongozi 41 wa hapa kwa kuchochea vita.

Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, Sudan Kusini imekuwa ikishuhudia vita ya kikatili ya wenyewe kwa wenyewe.

Ijumaa iliyopita, Mwenyekiti wa tume hiyo, Yasmin Sooka, alisema washukiwa wa vita nchini hapa wanapaswa kufunguliwa mashtaka ili waadhibiwe kisheria.

“Mahakama inaweza ikaandaliwa ili kushtaki waliochochea ghasia na vita,” alisema Sooka.

Kufikia sasa hakuna kiongozi yeyote mkuu serikalini nchini humo ambaye amefunguliwa mashtaka, licha ya Umoja wa Afrika (AU) kuahidi kufungua mahakama itakayowashughulikia viongozi waliohusika na vita.

“Kufuatia mkataba wa amani uliotiwa kati ya Sudan Kusini na Umoja wa Mataifa, viongozi hao hawastahili kuwa madarakani. Hii ndiyo njia ya kuokoa maisha ya wananchi walio hatarini,” alieleza Sooka.

Raia wengi wa Sudan Kusini, wakiwamo wa nchi nyingine, wamepoteza maisha kufuatia vita hiyo.

Utekaji nyara wa watu na uharibifu wa mali nchini humo umekuwa kama mazoea ya kila siku.

Sooka alifichua kuwa orodha ya washukiwa imewasilishwa kwa tume hiyo, tayari kwa mashtaka dhidi yao.

Rais Salva Kiir na wafuasi wake, wamekuwa wakipigana na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais, Riek Machar.

Kwa mujibu wa tume hiyo, baadhi ya wanajeshi wa viongozi hao wawili na wasaidizi wao wakuu, wanahusishwa na vita hiyo, ambayo pia imeshuhudia wanawake, watoto na hata wanaume wakibakwa.

Uamuzi huo wa UN unakuja siku chache baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya kushauri raia wake kuepuka kusafiri kwenda Sudan Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles