33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana wahimizwa kuamka na kujitambua

*Ni kupitia mpango salama wa kuwalinda

*Ubalozi wa Uswizi na UNFPA kuuzindua, Bara, Zanzibar kunufaika

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali ya Tanzania inatarajia kuzindua Mpango mpya unaolenga Vijana kuanzia umri wa miaka 10 hadi 24 lengo likiwa ni kuwasaidia kujitambua na kushiriki fursa zilizopo.

Afisa Programu wa Masuala ya Uzazi kwa Vijana Balehe kutoka Shirika la Umoja wa Matifa linaloshughulikia Idadi ya Watu na Masula aya Afya ya Uzazi(UNFPA) Tanzania, Fatina Kiluvia, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Aprili Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam na Afisa Programu wa Masuala ya Uzazi kwa Vijana Balehe kutoka Shirika la Umoja wa Matifa linaloshughulikia Idadi ya Watu na Masula aya Afya ya Uzazi(UNFPA) Tanzania, Fatina Kiluvia wakati akitambulisha mpango huo kwa wanahabari.

Fatina amesema kuwa mpango huo unaofahamika kama Mpango Salama wa kuwalinda Vijana ambao wanashirikiana na Ubalozi wa Uswizi nchini unatarajiwa kuzinduliwa Jumatatu Aprili 4, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako.

Amesema Mpango huo ambao utakuwa wa miaka mitatu kwa kuanza UNFPA kwa kushirikiana na wadau ikiwamo Serikali inalenga kuwawezesha vijana kushiriki katika vipaumbele vya ujenzi na maendeleo ya taifa.

“Vijana wengi wamekosa ushirikishwaji kutokakana na kutokuwa na elimu sahihi juu ya mambo mbalimbali ikiwamo elimu ya afya ya uzazi, kushindwa kujisimamia na kujitambua kwa ujumla hatua ambayo imekuwa ikichochea baadhi yao kujikuta wakiacha shule na hata wasichana kupata mimba katika umri mdogo na ndoa za mapema.

“Hivyo lengo la mradi huu ni kuona vijana wenye umri katika ya miaka 10 hadi 24 wanajengewa uwezo, tunaanza miaka mitatau ya awali lakini lengo ni kutekelezwa kwa miaka tisa,” amesema Kiluvia.

Aidha, katika hatua nyingine Kiluvia amehimiza Vijana na Watanzania kwa ujumla kuupokea mradi huo.

“Vijana na watanzania kwa ujumla nawasihi waupokee mradi huu kwani utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa letu kwani unaenda kusaidia kutengeneza Tanzania ya vijana imara zaidi.

“Mikoa ya awali itakayofikiwa na mradi huu kwa kuanza ni Dar es Salaam, Dodoma, Simiyu, Shinyanga na Kigoma, pia Zanzibar ambapo kila mkoa wilaya mbili zitafikiwa na mpango huu, hivyo tumaani kuwa kama ilivyo lengo la mradi huu utasaidia vijana kujitambua zaidi na kushiriki katika maamuzi ikiwamo kuwaepusha na hatari zikiwamo za maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI,” amesema Fatina.

Awali, akizungumzia mpango huo Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa, Ubalozi wa Uswizi nchini ambao ndio unafadhiri mpango huo, Leo Nascher, amesema lengo ni kuona ustawi kwa vijana wa Kitanzania kama ambavyo wamefanya kwenye mataifa mengine ya kusini mwa Afrika.

“Uswizi inaamini ustawi wa vijana wa kitanzania hivyo ndio maana ikaweka nguvu kubwa katika kuhakikisha kuwa wanajengewa uwezo wa kujitambua katika nyanja mbalimbali.

“Tunaamini kwamba ushirikiano wa muda mrefu ni muhimu, hivyo Ubalozi umejitolea kwa dhati kuendelea kuimarisha ushirikiano huu wa nchi mbali kuelekea kufikia malengo muhimu na kabambe ya kitaifa na kimataifa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UNFPA, Warren Bright, akizungumza kwenye ufunguzi wa hafla hiyo.

“Uswizi imetenga kiasi cha Dola 5,100,000 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa la Tanzania kwa siku za usoni, hivyo naamini kuwa wadau watauunga mkono,” amesema Nascher.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles