22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya CRDB yaombwa kutoa mikopo kwa wakulima Njombe

Na Elizabeth Kilindi, Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba ameiomba benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wingi kwa wakulima mkoani humo ili waweze kuzalisha kwa tija.

Kindamba ameyasema hayo jana wakati akizindua mabanda ya maonyesho kwa ajili ya mbio za mwenge wa uhuru ambapo amesema uwapo wa benki ya CRDB ni fursa kwa wakulima kwa sababu ya wa mikopo ya riba nafuu.

“Mkoa wetu ni mkoa wa wakulima, tunashukuru ujio wenu na napenda kuona sapoti yenu katika sekta ya kilimo, wananchi wa Njombe wengi ni wachapa kazi na kwa hiyo uwepo wenu na ujio wenu utakua na msaada mkubwa sana hasa kupitia mikopo,” amesema Kindamba.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Njombe, Amin Mwakangata amesema kuwa benki hiyo imetoa miamvuli 1,000 kwa ajili ya watoto wa halaiki, trakisut zaidi ya 1,000 na kugharamika ukarabati wa uwanja pamoja na kofia benki hiyo ikiwa ni mdhamini mkuu uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru aprili mbili.

Mwakangata amesema kuwa benki ya CRDB inafanya mambo mengi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi pamoja na Taifa.

“Benki yetu inashirikiana na serikali katika kuhakikisha makusanyo ya serikali yanafanyika kwa wakati, mifumo yetu ukiwa na akaunti ukiwa ni simbaking maana yake malipo ya serikali ya aina yoyote unaweza kulipa mahali ulipo,”amesema Mwakangata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles